Wananchi wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameshauriwa
kutoendekeza tabia za unyanyapaa kwa wagonjwa wanaoishi na virusi vya ukimwi
kwa kuwatungia majina mbalimbali kwani hakuna binadamu anayetambua aina ya kifo
atakachokufa nacho.
Akizungumza katika mkutano wa watendaji wa Serikali na
wajumbe wa uongozi wa kijiji cha Ludende wilayani hapa mganga mkuu wa Zahanati
ya Ludende Dkt. Zahao Mtafya amesema kuwa katika kata ya Ludende kuna zaidi ya
wagonjwa wa Ukimwi wanaochukua dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi
lakini kutokana na kuonekana waziwazi wakipanga foleni kuchukua dawa hizo jamii
inawanyanyapaa kwa kuwaita majina mbalimbali wasiyo yapenda.
Dkt. Mtafya amesema kuwa awali wagonjwa hao walikuwa katika
hali mbaya na wengine wamepoteza maisha kutokana na kunyanyapaliwa pia kata
hiyo kutokuwa na vipimo vya kupima CD4 lakini kwa sasa hali imeanza kutengamaa
kwa baadhi ya wagonjwa kwani Serikali kupitia mradi wa Tunajali wameweza
kununua mashine hiyo na huduma inaendelea pia wanaoishi na wagonjwa hao
wanapata elimu ya kupunguza unyanyapaa
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Ludende Bw.Vasco Mgimba
alikili kuwepo kwa tabia za unyanyapaa lakini aliwataka wanaotumia dawa za
kufubaza virusi vya ukimwi mara baada afya zao kutengamaa kuacha tabia ya
kusambaza virusi hivyo kwa makusudi kwa lengo la kulipiza visasi kwa
waliowanyanyapaa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment