Imeelezwa
kuwa mpango wa uzenzi wa maabala katika shule za Sekondari wilayani Ludewa
katika mkoa wa Njombe umekamilika kwa asilimia tisini kutokana na ukweli kwamba
idadi kubwa ya shule wilayani hapa zimekuwa na majengo ya kutosha hivyo kuwa
vyumba vya ziada ambavyo vimefanywa kuwa maabala hizo
Akitoa
taarifa ya mpango huo wa ujenzi wa maabara kwa waandishi wa habari jana ofisini
kwake Ofisa elimu wa shule za Sekondari
wilaya ya Ludewa Bw.Matenus Ndumbalo alisema mpango huo umefanikiwa kwa
asilimia tisini kwani katika shule za Sekondari wilayani Ludewa ni shule mbili
pekee ndizo zilizokosa vymba vya ziada.
Bw.Ndumbalo
alizitaja shule ambazo zimekosa vyumba vya ziada na kulazimika kuaandaa bajeti
ya ujenzi wa majengo mengine ya maabara ni pamoja na shule ya sekondari ya
Ketewaka na ile ya Makonde lakini nyingine zimekamilisha ukarabati wa vyumba na
tayari baadhi ya shule vifaa hivyo vya maabara vimeshawasili tayari kwa kuanza
kufundishia wanafunzi.
Alisema
kuwepo kwa vyumba vya ziada kumesababishwa na kupungua kwa idadi ya wanafunzi
katika shule hizo chanzo kikiwa ni mitihani ya kidato cha pili kwani
wanaoshindwa kufaulu hugoma kurudia kidato cha pili na kujikita katika shughuri
za kilimo hivyo madarasa hubaki wazi.
“Tumekuwa na
vyumba vya madarasa visivyo na kazi hali ambayo imeturahisishia kuvitenga
vyumba hivyo kwaajili ya maabara lakini bado tunachangamoto kubwa kwani kumekuwa
na idadi ndogo ya wanafunzi wanaopanda kidato cha tatu kutokana na kutofaulu
mtihani wa kidato pili na kufanya shule kuwa na idadi ndogo ya
wanafunzi”,alisema Ndumbalo.
Akitoa mfano
wa upungufu wa wanafunzi Bw.Ndumbalo
aliitaja shule ya Sekondari Ketewaka ambayo iko katika kijiji cha kimelembe
kata ya Nkomang’ombe kuwa ni moja ya shule zilizoathirika na mtihani wa kidato
cha pili hivyo kukasababisha wanafunzi wa kidato cha nne kufanya mtihani katika
shule nyingine.
Licha ya
kukamilisha kazi ya ujenzi wa Maabara kwa asilimia tisini pia alizitaja
changamoto zinazomkabili katika idara yake wilayani hapa ni pamoja na ukosefu
wa Walimu wa masomo ya Sayansi na walimu
wa kike katika baadhi ya shule ambazo zinadahalia.
Alisema
wilaya ya Ludewa ni moja ya wilaya zenye wanafunzi wenye vipaji kutokana na
kutumia vyakula vya asili na Samaki wa ziwa nyasa lakini wanashindwa kufanya
vizuri katika masomo ya sayansi kutokana na ukosefu wa walimu wa masomo hayo
hali ambayo imekuwa ni changamoto ya kila mwaka.
Bw.Ndumbalo alisema
licha ya kuwa katika baadhi ya shule ya Sekondari ujenzi wa maabara na vifaa
vyake umekamilika lakini hakuna walimu wa masomo ya Sayansi jambo ambalo bado
linawaumiza vichwa viongozi wa wilaya ya Ludewa pale wanapokutana katika vikao
ili kujadili hali ya Elimu katika wilaya.
Changamoto
nyingine ambayo imekuwa ikiitesa idara ya elimi ni ile ya ukosefu wa walimu wa
kike katika baadhi ya shule za sekondari na mfano wa moja ya shule hizo ni
shule ya Sekondari Makonde ambayo ina dahalia lakini haina mwalimu wa kike
ambaye angeweza kuwa jirani na wanafunzi wa kike hali ambayo inasababisha
walimu wa kiume kusikiliza matatizo ya wanafunzi wa kike.
Bw.Ndumbalo
alisema suala kuokuwa na walimu wa kike katika shule za Sekondari
limesababishwa na baadhi ya shule kutokuwa na Nyumba za walimu hivyo aliwataka wananchi kujitolea katika
ujenzi wa shule hizo ili walimu waweze kupata mahali pa kuishi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment