Mjumbe wa
Halmashauri kuu ya CCM Taifa(NEC) wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe
Bi.Elizabeth Haule amewataka viongozi waliochaguliwa na wasiochaguliwa katika uchaguzi
wa Serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni kuvunja makundi na kuendelea na
majukumu ya kulijenga taifa katika kipindi hiki cha sherehe za Chrismas na
Mwaka mpya.
Bi.Elizabeth
ameyasema hayo leo katika ofisi za CCM wilaya ya Ludewa wakati akiongea na
waandishi wa habari waliotaka kujua hali ya wagombe wa chama cha mapinduzi
ambao hawakuweza kuchaguliwa na wananchi na wengine walioshindwa katika kura za
maoni ndani ya chama.
Alisema hali
halisi ya wagombea walioshindwa uchaguzi katika kura za maoni na zile za
wananchi iko vizuri kwani asiyekubali kushindwa si mshindani hivyo haina sababu
ya kuendelea na makundi badala yake kukaa pamoja na kutekeleza majukumu ya
chama na Taifa kwa ujumla ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Bi.Elizabeth
alisema wilaya ya Ludewa inajumla ya vijiji 77 katika vijiji hivyo chama cha
Mapinduzi kimeweza kushinda nafasi ya uenyekiti wa vijiji 67 na vijiji 10
vimeweza kuchukuliwa na vyama vya upinzani hali inayoonesha kuwa chama cha
Mapinduzi kinakubalika na wananchi wa wilaya ya Ludewa na Taifa kwa ujumla.
“Tumeshinda
kwa kishindo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa ila ninachowaomba wanaccm
wenzangu kuvunja makundi ya uchaguzi uliopita na kukijenga chama kwaajili ya
kujiandaa uchaguzi mkuu mwaka 2015 pia nawaomba vijana wenzangu kuniunga mkono
mwakani kwa kuchukua fomu za kugombea nafasi za Udiwani”,Alisema Bi.Elizabeth.
Alisema
licha ya uchaguzi kumalizika bado kunabaadhi ya watu wanaendelea kukumbatia
itikadi za vyama hali ambayo si sahihi kwani katika msimu huu wa sikukuu ni
vyema kuweka itikadi za kisiasa pembeni na kusheherekea kwa pamoja kama
ilivyozoeleka katika tamaduni za kitanzania.
Bi.Elizabeth
alisema kumekuwa na wanasiasa wasio wa vumilivu hivyo wanaposhindwa kuchaguliwa
ama kukosa lidhaa kwa wananchi ya kushika uongozi huanza kuhama vyama na
kuvichafua vyama vingine mtu wa namna hiyo anakuwa hajakomaa kisiasa
kinachotakiwa ni kuwa watulivu na kujaribu kwa kipindi kingine.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment