RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UZAMIVU
Taasisi ya sayansi na teknolojia ya Nelson Mandela iliyopo mkoani
Arusha imemtunuku shahada ya heshima ya uzamivu rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dakta Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango wake
katika kukuza na uendelezaji wa sayansi na teknolojia hapa nchini.
Rais Dakta Kikwete ametunukiwa shahada hiyo ya heshima na mkuu wa
chuo hicho makamu wa rais Dakta Mohammed Gharib Bilal katika mahafali ya
pili ya chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Nelson Mandela ambapo
jumla ya wahitimu mia moja na sita wametunukiwa shahada zao kati yao
wahitimu tisini na tatu wakitunukiwa shahada za uzamili na kumi na tatu
shahada za uzamivu.
Akizungumza mara baada ya kutunukiwa shahada hiyo rais kikwete amesema.
Awali akizungumza kwenye mahafali hayo mwenyekiti wa baraza la chuo
hicho Profesa David Mwakyusa amesema hatua iliyofikiwa sasa ya ujenzi
wa maabara ni muhimu sana katika kuendeleza sayansi na teknolojia nchini
na kwamba upo umuhimu wa serikali kuwa na programu maalum ya kukuza
masomo ya sayansi ili maabara hizo ziweze kutumika na kufikia malengo.
Mahafali hayo pia yamehudhuriwa na naibu mkurugenzi mkuu wa shirika
la kimataifa la elimu, sayansi na utamaduni Gate Chewingida ambaye
anasema shirika hilo linatambua umuhimu wa chuo cha Nelson Mandela
katika maendeleo ya nchi za afrika na kwamba UNESCO itaendelea
kuzijengea uwezo nchi za afrika katika kufikia malengo.
No comments:
Post a Comment