Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Bi.Monica Mchilo akiwasalimia wahitimu
Bi.Monic Mchilo akiongea na wazazi
Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Ludewa Bw.Edings Mwakambonja akikumbatiana na muhitimu wakati akikabidhiwa cheti za kuzuia na kupambana na Rushwa
Mwakambonja akimpongeza muhitimu kwa kupata cheti cha kuzuia na kupambana na Rushwa
Bw.Madaha akimkabidhi cheti cha uthibitisho wa kuhitimu kidato cha nne mwanafunzi Stelah
Wahitimu akiwa katika picha ya pamoja
viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu
hawa ndio wahitimu wa kidato cha nne Ludewa Sekondari mwaka 2014
Mwanafunzi Stelah akimpatia zawadi ya Keki mama yake Mzazi kwa kumsaidia mpaka kufikia kidato cha nne
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon Mdaha akiwa katika picha ya pamoja na vinara wa masomo kwa kidato cha nne katika shule ya Ludewa Sekondari ambao walipata tuzo kwa kufanya vizuri katika masomo yao.
DC Madaha pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu
Stelah akipewa mkono wa pongezi na mwalimu wa wake aliyemfundisha shule ya msingi Ludewa Mjini.
Mkuu wa
wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Bw.Juma Solomon Madaha amewataka
wananchi wilayani hapa kutobeza shule za jumuhiya ya wazazi ccm Tanzania kwani
tokea awali ndizo zilizokuwa zikitoa elimu ya Sekondari bila kujari itikadi za
vyama vingine vya siasa nchini.
Bw.Madaha
aliyasema hayo katika hotuba yake hivi karibuni kwenye mahafari ya kidato cha
nne akiwa mgeni rasmi katika shule ya Sekondari Ludewa mjini ambayo inamilikiwa
na umoja wa wazizi wa chama cha mapinduzi ambapo shule hiyo awali ilikuwa na
wanafunzi zaidi ya 800 lakini hivi sasa inawanafunzi chini ya 400.
Alisema
shule hiyo imekuwa mkombozi katika wilaya ya Ludewa kwa kutoa elimu bora na
ufauru wa hali ya juu lakini kuna baadhi ya watu wanashindwa kupeleka watoto
wao eti kwa kua shule hiyo ni ya Chama Cha Mapinduzi dhana ambayo si sahihi
kwani hakuna chama cha siasa ambacho kimeanza kusoma kidato cha kwanza na
kuhitimu kidato cha nne.
Bw.Madaha
alisema hakuna shule ya Sekondari nchini ambayo inafundisha masomo ya chama cha
siasa hicho hayo ni mawazo mgando na yanapaswa kupigwa vita ili yasitengeneze
kasumba mbaya kwa watoto wanaohitaji elimu ili iwasaidie katika maisha yao.
“shule za
umoja wa wazazi wa ccm nchini hazifundishi masomo ya chama bali ni sirabasi za
wizara ya elimu hivyo wazazi mnapaswa kuzitumia shule hizi ambayo ni mkombozi
kwa maisha ya watoto wenu na hakuna chama ambacho kipo darasani zaidi ya watu
wakipata elimu ndio wanakwenda kuanzisha vyama vya siasa,hivyo tuache fikla
potofu zaidi ya kuawaendeleza watoto wetu”,alisema Bw.Madaha.
Aidha
mwenyekiti wa bodi ya shule ya Ludewa Sekondari na Diwani wa kata ya Ludewa
mjini Mh.Monica Mchilo aliwataka baadhi ya wanaume wenye tabia ya kuwarubuni
wanafunzi wa kike na kuwakatisha masomo kuacha mara moja tabia hiyo kwani ni
kinyume na maadiri ya kiafrika.
Alisema
kumekuwa na baadhi ya akina baba na vijana huwarubuni wanafunzi hao na baadae
kuwapa ujauzito na kuwatelekeza katika hali mbaya ya kimaisha bila ya kufikiria
kuwa nao wanamabinti kama hao ambao wako katika shule nyingine wakipata elimu
kama walivyo wa Ludewa Sekondari.
Mh.Monica
alisema kama kuna manaume anazipenda sana sketi za shule basi anaweza
kumnunulia mke wake azivae ili aongeze upendo kuliko kuwafuata watoto wa shule
na kuwaharibia ndoto zao za maisha.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment