Mkurugenzi wa AKWAYA Bw.Samwel Mputa akiongea na wananchi
Meneja wa kanda ya Nyanda za juu kusini wa PANITA Bw.Aloyce Millinga akiongea na wananchi
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha akihutubia wananchi
Vijana wa IVA YOUTH GROUP wakilishambulia jukwaa
Mkuu wa wilaya akigawa chakula kwa familia zisizo na uwezo
Wapishi wakiwajibika
picha ya pamoja ya viongozi
watoto wakipa chakula cha mchana
Shirika
lisilo la kiserikali la AKWAYA linalojihusisha na shughuri za kijamii kwa
Wagane,Wajane na Watoto yatima wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe limeanza
kutekeleza mpango wa kupunguza tatizo la utapiamlo ambalo limekithiri wilayani
hapa kwa kutoa elimu kwa wazazi kuweza kufanya matumizi bora ya chakula.
Akiongea na
wananchi katika tamasha lililoandaliwa na shirika hilo jana Ludewa kijijini
Mkurugenzi wa AKWAYA Bw.Samwel Mputa alisema wialaya ya Ludewa imejaliwa kuwa
na rutuba nzuri inayostawisha mazao ya chakula aina zote lakini inashangaza
kuona hali ya utapiamlo iko juu.
Bw.Mputa
alisema mpaka sasa takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya 52% ya watoto waishio
mkoani Njombe wanatatizo la utapiamlo,hali
hiyo inasababishwa na wazazi kushindwa kupanga matumizi bora ya chakula kwani
muda mwingi wamekuwa wakiwaacha watoto wajihudumie wakati wao hushinda katika
vilabu vya pombe.
Alisema
tamasha hilo ambalo limefadhiliwa na PANATA
na SAVE THE CHILDREN linalengo la kufanya uhamasishaji juu ya matumizi
bora ya chakula ili kuondoa tatizo la utapiamlo kwani wako baadhi ya wazazi
bado wajawa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi bora ya chakula hasa rishe bora
lakini kupitia matamasha ambayo yanajumuisha vikundi vya sanaa na vyombo vya
habari wananchi wanaweza kupata uelewa kuhusu rishe bora.
“Utapiamlo
uko katika aina nne ambazo ni uzito pungufu chini ya kg2.5,udumavu,ukondefu na
uzito chini ya ule maalumu wa kuzaliwa
hali ambayo ni hatari kwa afya ya mtoto kwani hata baadhi ya wazazi
hawazingatii mlo kamili hivyo kupelekea kuzaa watoto wa aina hiyo lakini sisi kama akwaya tumejipanga
kupunguza na kama si kutokomeza tatizo hilo wilayani Ludewa”,alisema Mputa.
Mgeni rasmi
katika tamasha hilo ambaye ni mkuu wa wilaya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha
katika hotuba yake alisisitiza kuwa wilaya yake haina tatizo la chakula lakini
wananchi wake bado hawana mpangilio mzuri wa matumizi ya chakula bora hivyo ni
vema viongozi wa vijiji na wale wahudumu wa afya ya msingi kutoa elimu hiyo
wakati wa vikao vya vijiji ili kupunguza tatizo la utapiamlo.
Bw.Madaha
alilimwagia sifa shirika la akwaya kwa kuanzisha mpango huo ambao utaleta
mabadiriko katika jamii na kuwataka wananchi wa wilaya ya Ludewa hususani mkoa
wa Njombe kuacha kujizolea sifa mbaya
nchini kwani janga la ukimwi mkoa wa Njombe unaongoza pia utapiamlo
siafa ambazo si nzuri kwa mikoa mingine.
Aidha meneja
wa PANITA nyanda za juu kusini Bw.Aloyce Millinga aliitaka Serikali kutoa
ushirikiano kwa mashirika yasiyo ya kiserikali katika miradi mbalimbali
iliyaweze kushiriki ipasavyo katika kuihudumia jamii.
Alisema
baadhi ya viongozi wa Serikali wamekuwa kikwazo kwa mashirika hayo pale
yanapotaka kuwahudumia wananchi kwa kutokuwa na takwimu sahihi zinazohusu
maendeleo ya jamii na hali ya chakula kwa ujumla.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment