Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha akisoma hotuba ya kufunga mafunzo ya mgambo kata ya Mkongobaki
Mkuu wa wilaya akikagua gwaride
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha akimkabidhi zawadi ya Jumla Asha Mohammed bint pekee aliyefuzu mafunzo hayo
Bw.Madaha akatikati akiwa na Diwani wa kata ya Mkongobaki Mh.Alfred Mtweve pamoja na mshauri wa mgambo wilaya ya Ludewa Meja Ngingi
Mkuu wa
wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Bw.Juma Solomon Madaha amewataka vijana
wilayani hapa kutoyakimbia mafunzo ya jeshi la Mgambo kwani ni mazoezi ya
ukakamavu ambayo mwisho wa siku yanakuwa ajira ya kudumu katika makampuni
mbailimbali ya ulinzi.
Bw.Madaha
aliyasema hayo jana katika kata ya Mkongobaki wakati wa akiyafunga rasmi
mafunzo ya jeshi la Mgambo 29 akiwemo mwanamke mmoja ambapo changamoto kubwa aliyoelezwa na
wakufunzi ni baadhi ya vijana kutimua mbio wakati wa mafunzo na kuhama kabisa
kwa kuogopa mazoezi.
Akihutubia
umati wa wananchi ambao ulifulika katika viwanja vya Mkongobaki Bw.Madaha
alisema jeshi la mgambo ni muhimu sana katika ulizi wa jamii lakini inashangaza
kuona baadhi ya vijana kuyakimbia
mafunzo hayo ambayo ni moja ya ajira hasa kwa kipindi hiki cha uanzishwaji wa
migodi ya madini wilayani Ludewa.
Alisema
makampuni ya wachimbaji wa madini hayo watahitaji walinzi hivyo ni vyema vijana
wakaandaliwa ili kunufaika na fulsa za ajira katika migodi hiyo na kuacha tabia
ya kuwa watazamaji wa migodi yao pale walinzi wanapotafutwa wilaya nyingine na
kuajiriwa kwa mishahara minono.
“Jeshi la
Mgambo ni chombo cha ulinzi kinachotambulika nchini hivyo vijana mnaohitimu
mafunzo haya leo mnapaswa kukaa pamoja na kufungua kampuni yenu ya ulinzi na
kuisajiri na sisi tutakuwa watetezi wenu pale ambapo wawekezaji watahitaji
walinzi hatutaruhusu kampunui za ulinzi za nje ya wilaya hii zikapata kazi
wakati nyie mpo”,alisema Mh.Madaha.
Naye Diwani
wa kata ya Mkongobaki Mh.Alfred Mtweve aliushukuru uongozi wa wilaya ya Ludewa
kupeleka mafunzo hayo katika kata yake kwani vijana wa kata hiyo watanufaika na
fulsa za ajira katika migodi hiyo mikubwa inayotarajia kuanzishwa na wawekezaji
wa ndani ya nchi wa wale wa nje.
Mh.Mtweve
alitoa sifa nyingi kwa binti pekee aliyejulikana kwa jina la Asha Mohammed kwa
kuhudhuria mafunzo hayo mpaka mwisho licha ya kuwa kuna wengine walikimbia
baada ya kuona ugumu wa mazoezi hivyo aliuomba uongozi wa wilaya kumfikilia
binti huyo pale zinapotokea ajira za ulinzi katika ofisi mbalimbali za wilaya.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment