Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

August 22, 2014

WATOTO WA KIPAIMARA KATIKA KANISA LA ANGLICAN WILAYANI LUDEWAWAFANYA ZIARA YA KUWAFARIJI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA LUDEWA


mtoto wa kipaimara akimwona mgonjwa



akina mama wakiwa katika shughuli zao



watoto wakiwa pamoja na zawadi za kuwafariji wagonjwa





Watoto wanaoyarajiwa kupata kipaimara mwaka huu katika kanisa la watakatifu wote Wilayani Ludewa Mkoani Njombe dayosisi ya south west tanganyika wamefanya ziara ya kuwafariji wagonjwa mbalimbali katika Hospitali ya wilaya ya ludewa   .
Katika ziara hiyo ya kuwafariji wagonjwa watoto hao walipata Baraka zote kutoka kwa kasisi wa kanisa kuu la watakatifu wote Mch.Mtweve ambapo aliwaasa waumin wa kanisa hilo  kutoa sadaka kwa ajiri ya kumpeza MUNGU na sio binadamu 
Pia ameongeza kuwa ni vyema kwa waunin na wananchi wote wialyan hapa kujenga tamaduni za kwenda kuwafariji na kuwaona wagonjwa kila mara kwani kufanya hivyo kunawapa faraja wagonjwa na pia kunawaongezea dhawabu mbele ya mwenyezi MUNGU.
Watoto hao waliongozana na Mwal.wao Azali Haule ambapo
Kwa upande wa wauguzi wa hospitali ya wilaya ya Ludewa wamewashukuru kwa moyo wa dhati watoto hao pamoja na kanisa nzima la watakatifu wote lilipo ludewa kwa kitendo hicho cha kuwafariji wagonjwa.
Kwa upande wa wagonjwa hao pamoja na akina mama wajawazito waliopo katika wodi maalum ya kuwatunzia akina mama hao wameshukuru kiujumla wototo hao .alisema mama mmoja aliyekuwa wodin hapo



Jivunie kuwa mwana ludewa

No comments: