jeneza ambalo mwili wa Ibrahim ulihiofadhiwa
Wananchi walioandamana kuhakikisha Mbwa hao wanauawa
Mbwa baada ya kuuawa
Mbwa baada ya kuuawa
Na Bazil Makungu Ludewa
na Nickson Mahundi
Wananchi wa kata ya Ludewa
wameungana pamoja kufanya maandamano ya kushinikiza mbwa waliomuua
mtoto na kumtafuna wanauawa baada ya mmiliki wa mbwa hao kutishia
kuwashtaki watakao husika kuwaua mbwa wake.
Wakizunguimza kwa nyakati
tofauti katika mkutano wa dharula ulioitishwa na Diwani wa kata ya
Ludewa Mama Monica Mchilo walisema Mbwa hao wamekuwa tishio kwa muda
mrefu kwani wameshateketeza mifugo mingi wakiwemo mbuzi lakini cha
kushangaza kila wanapolipeleka suala hilo katika vyombo vya dola
mmiliki huwaeleza walete ushahidi.
Hali hiyo imejitokeza tena
kwa mmiliki wa mbwa hao alipoelezwa kuwa wamefanya mauaji na kumla
mtoto wa darasa la tatu katika shule ya msingi Ludewa mjini
aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Chipungahelo(9)aliwataka wananchi
kuleta ushahidi licha ya kuwa Askari wa jeshi la polisi kwa kutumia
silaha na kuuokoa mwili wa mtoto huyo ukiwa tayali umeshaliwa katika
baadhi ya viungo.
Akiongea katika mkutano
huo mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ludewa Bw.Omary Kiowi
alisema tukio na kauli za mmiliki wa Mbwa hao wawili Bw.Bosco
Lingalangala hazivumiliki kwa wanaludewa kwani amekuwa akiwatishia
wananchi kwa kutumia bastola kila wakati hivyo kikao hicho kiliamuru
mbwa hao wauawe na mmiliki achukuliwe hatua za kisheria.
“Tokea nizaliwe zijawahi
kuona Mbwa akitafuna mtu, hii ni mara ya kwanza,hatuwezi kuvumilia na
ninachokiomba wananchi msifanye fujo naamini tukitoka hapa kwa
kushirikiana na ofisi ya mifugo pamoja na jeshi la Polisi tunakwenda
kumuua mbwa aliyebaki na tunamtaka Bw.Bosco atushtaki wananchi wote
na Serikali yetu kwa sababu anadhani yeye yuko juu ya sheria”,alisema
Bw.Kiowi.
Kufuatia kauli za vitisho
wananchi wakaomba kikao kiahirishwe na kuanza maandamano kuelekea
katika nyamba ya mmiliki wa mbwa hao ambako aliuawa marehemu Ibrahim
na kuhakikisha wananmuua mbwa aliyebaki kwa kupigwa risasi,kwa
hasira walizo kuwa nazo wananchi hao waliamua kuondoka na Mbwa hao
wote wawili wakiwa wamekufa na kupita nao mitaani huku wakiimba
nyimbo mbalimbali.
Baada ya kuzunguka na
mizoga ya mbwa hao mitaani kwa muda mrefu hatimaye walielekea katika
ofisi ya kata na kuamua kuwachoma moto na kuwateketeza kabisa na
kuendelea na kikao ambacho kiliibua shangwe na vifijo baada ya mzee
Laurance Mtweve (Muhuchu) ambaye ni mzee mashuhuri kutoa kauli ya
kuutaka uongozi wa kijiji kumuandikia barua mkuu wa wilaya ya Ludewa
ya kufukuza Bosco kuishi eneo la Ikilu kutokana na vitisho vyake.
Mzee Muhuchu alisema kama
uongozi wa wilaya utashindwa kufanya hivyo basi wazee wa wilaya ya
Ludewa watamuandikia barua Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kuwa wamechoshwa na unyanyasaji wa Bw.Bosco
hiyo hawamuhitaji wilayani hapa tena.
Alisema kwani imekuwa
kawaida yake kuwatisha wananchi kwa kutumia bastola hali inayowafanya
wananchi kuishi kwa kuhofia usalama wao kwani inaonekana yuko juu ya
sheria kutokana na kufanya matukio ya ajabu lakini wanaoshtaki
hupuuzwa na jeshi la polisi hapa Ludewa.
Aidha Diwani wa kata ya
Ludewa kupitia CCM mama Monica Mchilo aliwataka wananchi kupunguza
jazba wakati sheria inachukua mkondo wake ingawa awali alionesha
kutoridhishwa na kauli za mmiliki wa mbwa hao kuwa atawashtaki
watakaohusika kuwaua.
Mama Mchilo alisema hakuna
aliyeridhishwa na kauli mbaya za Bosco lakini anaamini Serikali ni
sikivu itasikia kilio cha wananchi wa kata ya Ludewa kutokana na
vitisho vya mtu huyo ambaye hana hata chembe ya utu kwa kusema mbwa
wasiuawe bali atawalipa fidia wafiwa.
Aliwashukuru wananchi kwa
kufanya maandamano ya amani ambayo hayakuleta madhara kwa jamii
lakini yalifanikisha kuwaua mbwa ambao walikuwa ni tishio kwa jamii
hasa kwa wanafunzi wanaopita eneo hilo ambako aliwafugia mbwa hao.
No comments:
Post a Comment