Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

August 13, 2014

WAKULIMA LUDEWA WAHOFIA SERIKALI KUTONUNUA MAHINDI YAO.

Baadhi ya wakulima ambao hufika kila siku katika eneo walilohifadhia mahindi yao wakisubiri SGRF kwa kununua mahindi hayo bila mafanikio
hii ni baadhi ya shehena ya mahindi ambayo yanasubiliwa kuuzwa ysliyoko katika godauni la kata ya Ludewa mjini

eneo la Ghara likiwa limejaa mahindi kuanzia ndani hadi nje lakini wakala wa Serikali wa kununua mahindi hayo bado hawajatokea na bado haijulikani ni lini watakuja kuyanunua mahindi hayo kwa wakulima wilayani Ludewa.

wadau mbalimbali wa kilimo wamekuwa wakitembelea eneo hilo kuona hali halisi ya shehena ya mahindi huku mengine yakiwa bado mashambani

Vijana wakilinda mahindi yao kila siku wakisubiri kuyauza

      Bw.Kidulile akionesha shehena ya mahindi inayoendelea kuletwa na kukosa eneo la kuyaweka

Wakulima wilayani Ludewa wamekata matumaini ya kuyauza mahindi yao kwa wakala wa Serikali kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi inayoonesha ni lini wanunuzi hao watafika na kuanza kuyanunua hali ambayo imesababisha baadhi ya wakulima kushindwa kuendelea na uvunaji wa mahindi ambayo bado yako mashambani.

Akiongea na mwandhishi wa habari hii mkulima mmoja aliyejitambulisha  kwa jina la Noa Kidulile alisema tayali eneo hilo la Ghara la mahindi nimeshajaa kuanzia ndani hadi nje lakini hakuna kinachoendelea, awali taarifa zilienea kuwa mahindi hayo yangeanza kununuliwa na Serikali kuanzia tarehe 8 Agost mwaka huu lakini mpaka leo hakuna ununuzi unaoendelea.

Bw.Kidulile alisema wakulima wameshaanza kuwa na mashaka dhidi ya hatima ya mahindi yao licha yakuwa mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe kuwatangazia wakulima hao siku ya mbio za mwenge wa Uhuru kuwa Serikali imetenga fedha za kununulia mahindi hivyo mapema mwezi Agosti yangeanza kununuliwa.

Alisema imefikia wakati wakulima wamekuwa wakikesha katika ghara ili kuwasubiri wanunuzi hao ikiwa hayo ni baadhi tu ya mahindi kwani bado wakulima wanamahindi ya mwaka 2013 ambayo Serikali ilishindwa kuyanunua na mengine bado yako mashambani hayajaletwa hapa na tayari eneo la kuhifadhia mahindi limeshajaa sasa hatma ya mahindi haya bado haijajulikana kama yatanunuliwa yote au itakuwa kama mwaka jana.

"Ndugu mwandishi nadhani umeona mwenyewe hali halisi ya shehena ya mahindi yetu na haya ni sehemu tu lakini bado mzigo halisi kutoka mashambani haujawasili hapa na kila mmoja anamashaka kama Serikali itaweza kuyanunua yote au la na kama haitayanunua yote je tutayauza wapi? ninachokiomba ikiwezekana mipaka ya nchi ifunguliwe ili tuuze nchi za jirani na si kuyaona yakiozea hapa",alisema Kidulile.

Bw.Kidulile alisema anaipongeza Serikali kwa kutoa pembejeo za kilimo(Ruzuku) lakini ununuzi wa mazao hayo ni muhimu hivyo anaiomba Serikali itoe tamko kuhusiana na mahindi hayo kama yataweza kununuliwa yote ili wakulima waanze kujipanga na msimu mwingine wa kilimo ambao pia unatarajia kugharimu fedha nyingi za wakulima.

Aidha afisa kilimo wilayani hapa Bw.Kelvin Mbena alikili kuwepo kwa shehena kubwa ya mahindi katika maghara yote ya wilaya ya Ludewa na kuwataka wakulima kuwa watulivu kwani Serikali kupitia wakala wake wa ununuzi wanatarajia kuyanunua mahindi hayo kwa wakulima na kuyahifadhi.

Bw.Mbena alisema taarifa alizonazo katika ofisi yake ununuzi wa mahindi hayo utaanza tarehe 15 Augast mwaka huu katika vituo vyote hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi wa kuyauza mahindi hayo kwa baadhi ya wakulima wanavyo fikiri,jambo la msingi ni kuyaandaa mahindi hayo kwa kuyasafisha vizuri ili siku ikifika yasiwe na dosari.

Aliwasisitiza wakulima ambao bado hawajayavuna mahindi yao waendelee na uvunaji kutokana na hali halisi ya wilaya ya Ludewa katika msimu wa kiangazi kuna baadhi ya watu waharibifu wa mazingira hutorosha moto ambao huteketeza misitu na baadhi ya mali za wananchi.

Endelea kufuatilia katika mtandao huu nini kimejiri katika ununuzi wa mahindi hayo.

No comments: