Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

August 17, 2014

MBUNGE FILIKUNJOMBE NA MNG'ONGO' WASIMIKWA KUWA WALEZI UWT MKOA WA NJOMBE


Deo Filikunjombe na Lediana Mng'ongo wakionesha katiba mara baada ya kusimikwa

Mbunge wa Jimbo la Ludewa, mkoani Njombe, Deo Filikunjombe na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Iringa, Lediana Mng’ong’o jana wamesimikwa kuwa walezi wa  Umoja wa Wanawake UWT mkoa wa Njombe mara baada ya kuchaguliwa rasmi na umoja huo.

Zoezi hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Turbo uliopo mjini hapa, ambapo pamoja na mambo mengine mbunge Filikunjombe ametoa fedha taslimu shilingi milioni 10 kwa ajili ya kusaidia kununua gari litakalofanya kazi ya kuwatembelea wanachama wa UWT katika sehemu mbalimbali za mkoa wa Njombe.



Akizungumza na wanawake wa jumuiya ya (UWT) wakati akitoa shukrani zake za kuwa mlezi wa jumuiya hiyo,  Filikunjombe aliwataka  wakina mama hao kuhakikisha wanashikamana kwa pamoja ili kuhakikisha Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia UWT kinasonga mbele kiuchumi, kimaendeleo na hata kisiasa.

Mbunge Filikunjombe aliwataka wakina mama hao kupitia jumuiya hiyo, kuhakikisha wanazungumza na vijana majumbani kuacha tabia ya kukaa vijiweni na badala yake wajishughulishe.

“Nawasihi mimi ni kijana bado na nyie ni wakina mama, nyie ni wazazi, mmetulia sisis vijana, mnapokwenda kule majumbani, tuzungumze na wachama wetu, tuzungumze na vijana tuache kukaa na kulalamika, kila mmoja atomize wajibu wake,naamini nyie wakina mama mkisema kwa huruma,kwa upendo huenda vijana wenzangu watawaeleweni,” alisema Filikunjombe.

“Vijana wengi sasa hivi hawafanyi kazi, wanakaa kijiweni na kazi yao ni kunung’unika na kulalamika tu, wanasubiri serikali ifanye kila jambo, hii haiwezekani, serikali ni nani, ni sisi wenyewe,” aliongeza Filikunjombe.


Kwa upande wake Mbunge wa Mwibala mkoani Mara, Kange Lugola aliyeambatana na Filikunjombe ameahidi kuitisha semina ya siku tatu mkoani Njombe kwa ajili ya jumuiya hiyo ya wanawake lengo likiwa ni kuirudisha Kata ya Njombe Mjini inayoshikiriwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Diwani wake Agrey Mtambo.

“Kama Chama cha Mapinduzi katika mkoa wa Njombe, nyinyi malezi yenu yatakuwa mabovu, kwa sababu malezi mazuri ni yale yanayoleta matunda na matunda haya yaanzie Njombe Mjini ambapo wenzetu mmewapa Kata moja ndipo malezi yaanzie, na mimi naahidi nitakuwa bega kwa began a nyie,” alisema Lugola

Lugola pia aliahidi kuendelea kushirikiana na wanawake wa jumuiya hiyo li waweze kupambana na changamoto mbalimbali zilizopo ndani ya chama hivi sasa.

“Nitashirikiana na nyie akina mama na walezi wenu kuhakikisha kwamba wakina mama mnaimarika ili msaidie CCM,” alisema Lugola.

Wakati huohuo, Mjumbe wa Baraza la Wanawake mkoani Njombe, ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Dk. Suzan Kolimba alitoa shilingi milioni 5 fedha taslimu kwa ajili ya kusaidia Jumuiya ya Wanawake (UWT) mkoani Njombe.

No comments: