Huyu ndiye Mbwa aliyemtafuna mtoto Ibrahim akishirikiana na mwingine ambaye mmiliki amegoma kuuawa na kuahidi atawafungulia mashtaka waliomuua mbwa wake
Hili ndilo endeo ambalo marehemu Ibrahim alitafunwa na Mbwa
Wananchi wakimzika marehemu Ibrahim aliyeuawa na Mbwa
Diwani wa kata ya Ludewa mama Monica Mchilo akiongea makaburini na wananchi baada ya mazishi ya Ibrahim
Baba wa marehemu Ibrahim Bw.Faraja Chipungahelo akiwa na masikitiko ya kifo cha mwanae
Baba na mama wa marehemu Ibrahim wakiweka taji la maua katika kaburi la mtoto wao aliyeuawa na kuliwa baadhi ya viungo na Mbwa.
Shangazi wa marehemu wakiweka taji la maua
umati uliofulika katika mazishi ya Ibrahim Chipungahelo
Wananchi wa Mji wa Ludewa katika mka wa Njombe wameingia katika mgogolo mkubwa na viongozi wao wa Serikali baada ya Mmiliki wa Mbwa wawili waliosababisha kifo cha mtoto Ibrahim Chipungahelo Bw.Bocso Lingalangala kumweleza Diwani wa kata ya Ludewa mjini kupitia CCM Mh.Monica Mchilo kuwa atakeyewaua Mbwa hao atamshtaki.
Akiongea kwa uchungu Diwani huyo baada ya mazishi ya marehemu Ibrahimu alisema tayari Mbwa mmoja ameshauawa kwa kushirikiana na afisa mifugo pamoja na Jeshi la Polisi lakini chakusikitisha wakiwa katika harakati za kumuua mbwa aliyebaki alishangazwa na kitendo cha askari polisi kuondoka eneo la tukio na kuwaacha wananchi wakiwa na bwana mifugo.
Mh Monica alisema mara baada ya kuondoka Polisi hao wakidai wamepewa amri na mkubwa wao kuwa waondoke eneo hilo haraka ndipo akapokea simu kutoka kwa mmliki wa Mbwa hao ambaye anaishi Jijini Dar es Salaam akimtaka kuondoka na wananchi eneo hilo na kutomuua mbwa aliyebaki kwani mbwa hao amewanunua nchini Marekani kwa gharama kubwa hivyo anatarajia kuja na mwanasheria wake kuwashtaki waliyomuua huyo mmoja.
Diwani huyo alisema amri ya kuwaua Mbwa hao ilitolewa na Mkuu wa wilaya ambaye yuko safarini kwani yeye ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya ya Ludewa hivyo jeshi la polisi limekiuka maagizo ya kiongozi wa wilaya hali ambayo ni hatari hivyo kama Jeshi la Polisi linakiuka maagizo ya mkuu wa wilaya na kumsikiliza raia wananchi wanatakiwa kujua kuwa wanatakiwa kujilinda wenyewe bila kitegemea jeshi hilo wilayani Ludewa.
Mbwa hao wawili walimvamia marehemu Ibrahim Chipungahelo(9) Oktoba 8 mwaka huu ambaye alikuwa akisoma darasa la tatu katika shule ya msingi Ludewa Mjini na kumuua na baadaye kumtafuna katika baadhi ya viungo majira ya saa saba mchana hali ambayo imesababisha wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo katika shule hiyo kwa kuhofia mbwa mmoja aliyebaki hai baada ya mmoja kuuawa.
"Wananchi inashangaza Mbwa wamemuua mtoto wakini Bosco anasema yeye anawanasheria wake hivyo atafungua kesi kwanini tuwauwe mbwa hao,na tunauhakika gani kama ndio waliomuua huyu mtoto na kasema tungemweleza atulipe na si kuwaua,hivi thamani ya mtu inaweza kufananishwa na mbwa?nashangaa hata jeshi la polisi wilayani hapa kutoshirikiana nasi kwa tukio hili wanadai wamezuiwa na OCD hivi hii ni haki?"aliuliza Mh.Monica wakiwa makaburini kwa mazishi.
Hali hiyo iliamsha hasira kwa wananchi ambao wameulalamikia uongozi wa jeshi la Polisi wilaya ya Ludewa na Serikali ya wilaya kwa kutowalinda wananchi na kuwakumbatia watu wachache wasio na uchungu wa maisha ya watanzania hivyo wananchi wao walikaanza kuondoka makabulini wakiwa na lengo la kwenda kuichoma moto nyumba Bosco ambako Mbwa hao wanaishi.
Mh.Monica aliwasihi wananchi wasifanye hivyo kwani aliwatangazia viongozi wa vyama vya siasa,wakuu wa madhehebu ya Dini,viongozi mbalimbali na wazee mashuhuri kukutana katika ofisi ya kata kwa kikao cha dharula ambacho kitatoa tamko,kwani nyumba hiyo iko karibu na nyumba anayoishi mkuu wa wilaya ni baadhi ya nyumba zilizopo ndani ya Ikulu ya wilaya ya Ludewa ambazo zimeuzwa hivyo kwa kuichoma moto kunaweza kusababisha madhara makubwa zaidi.
Aidha akihojiwa kwa njia ya simu ya kiganjani na mwandishi wa habari hii mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha alisema yuko safarini Mkoani Mtwara katika kikao hivyo hakutoa kibali cha kutouawa kwa mbwa hao kama watu wanavyofikili.
Bw.Madaha alisema kazi ya kuwaua mbwa wenye kichaa ni kazi ya Maafisa nifugo na si Jeshi la polisi lakini kama kunaulazima wa msaada katika hilo Jeshi la Polisi linatakiwa kusaidia kufanya kazi hiyo kwani Mbwa hao wanaweza kusababisha madhara mengine ambayo yanaweza kuleta uvunjifu wa amani wilayani hapo.
Mpaka Mwandishi wa habari hii anakenda mtamboni juhudi za kumpata mmiliki wa mbwa hao ziligonga mwamba na bado wananchi wenye jazba walikuwa wakisubiri maamuzi ya kikao ambacho kimeitishwa na Diwani wao Mh.Monica licha ya kuwa miliki wa Mbwa hao kuwapigia simu baadhi ya watu na kuwatisha kwa Bastola ambayo anaimiliki.
mwisho.
No comments:
Post a Comment