Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

August 10, 2014

FILIKUNJOMBEA AVUTIWA NA DIWANI WA CHADEMA KUTEKELEZA ILANI YA CCM ,AMPA ZAWADI YA KOFIA YA CCM

Mradi  huu umeanzishwa na diwani wa Chadema kata  hiyo
Filikunjombe  akiongea  kabla ya  kumzawadia kofia diwani Mlelwa
Mbunge Filikunjombe akizunguma baada ya kumzawadia kofia yake  diwani wa kata ya Mlangali Faraja Mlelwa

MBUNGE wa jimbo la  Ludewa  Deo  Filikunjombe amempongeza  diwani  wa kata ya Mlangali  kupitia  chama  cha  Demokrasia na maendeleo ( chadema ) Faraja Mlelwa  kwa  hatua yake  ya  kuweka  itikadi  ya  vyama  kando na  kushiriki katika  utekelezaji wa ilani ya CCM.

Kuwa hatua ya  diwani  huyo  kushughulikia  kero ya maji kwa  kuwafikishia maji ya bomba  wakazi wa  kitongoji cha Madindu  kata ya Mlangali ni jambo njema na ni mfano  wa  kuingwa  kwa  wapinzani wengine  ambao siku  zote wao ni mabingwa  wa  kuhamasisha  wananchi  kutoshiriki maendeleo.

Akizungumza  jana wakati  wa  uzinduzi  wa  mradi  huo wa maji ambao umegharimu  zaidi ya milioni 4.7 na  diwani  huyo kuchangia kiasi cha Tsh 500,000 kuunga nguvu kazi  za  wananchi ,mbunge  Filikunjombe  alisema  kuwa uamuzi  wa  kuibua mradi  huo ni uamuzi wa  kizalendo .

Kwani  alisema  wazo  hilo la kuwa na mradi  wa maji ili  kuondoa kero ya maji katika kitongoji  hicho  ilibuniwa na mwenyekiti  wa  serikali ya  kijiji  pamoja na diwani  huyo   japo awali mradi  wa  maji katika  eneo  hilo kwa  kuwatumia  wataalam  wa  Halmashauri  mradi  huo  wa maji  ungetumia  zaidi ya  Tsh milioni 80.

" Nimeelezwa  kuwa  walikuja  wataalam wa  maji  kutoka  Halmashauri ya  Ludewa na kuchora  mchoro wa  mradi  huo na makisio ya mradi  mzima  na ili  watu  waweze kupata maji ilikuwa ni Tsh milioni 80 fedha  ambazo zisingepatikana  kwa  sasa  na hivyo  wananchi  wangekuwa  hawana  huduma  hii  ya  maji ....mimi huyu diwani si  wa  chama  changu ni mpinzani ila katika  hili namuunga mkono "

Pia  alisema  ataendelea  kuungana na  diwani   huyo  kuwasaidia wananchi  wake  kwani  diwani Mlelwa ameonyesha  kutekeleza  ilani ya  CCM na mbali ya  kuwa yeye kama mbunge  na  diwani huyo vyama  tofauti  bado ameamua kumwalika  kuzindua  mradi  huo.

Filikunjombe  alisema  kuwa mahitaji  mengine  ambayo yanahitajika katika mradi  huo  likiwemo tenki  ya  kuhifadhia  maji la  lita 5000 atalinunua pamoja na  kuanzisha  ujenzi  wa tenki la kudumu ambalo  litahifadhi maji  zaidi ya lita 10,000

Hivyo  alisema  kuwa  kazi  ya  ujenzi  wa  tenki   hilo anataraji  kuongoza  mwenyewe  siku ya tarehe  17  mwezi  huu kwa  kufika  kijijini  hapo  kushiriki shughuli ya  ujenzi  wa  tenki  hilo kama  sehemu ya  kuunga mkono jitihada  hizo  za  diwani na  wananchi  katika  kujiletea maendeleo.

Hata  hivyo alisema  kuwa mahitaji ya  wananchi  hao ambao walikuwa na kero  kubwa  ya maji si  serikali tatu ama katiba  mpya  bali  mahitaji  yao yalikuwa ni maji na kero  nyingine  zinazowakabili .

Diwani  wa  kata  hiyo Bw Mlelwa mbali ya  kumpongeza  mbunge  huyo  kwa  kuahidi  kuwaunga mkono katika  ujenzi wa tenki hilo bado  alisema ataendelea  kufanya  kazi kwa  karibu na mbunge  huyo bila  kutangulia itikadi za  chama  chake .

No comments: