Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

July 28, 2014


NGOYE AWAPIGIA MAGOTI WANALUDEWA, KOMBA AHIMIZA MSIMAMO, LUGOLA AWATAKA WAACHE MICHEPUKO WABAKI NJIA KUU.

 Filikunjombe akiongea na wajumbe kutoka jimboni kwake wilayani Ludewa
 Filikunjombe akiwa na Hilda Ngoye pamoja na Kapten Komba

 kapten Komba mbunge wa Nyasa akiimba nyimbo za chama cha Mapinduzi
     Mbunge wa Mbinga Gaudens Kayombo akiongea na wajumbe kutoka wilaya ya Ludewa

WABUNGE wa chama cha mapinduzi (ccm) na wale wa upinzani wameendelea kutoa mawazo, maoni na hisia tofauti kufuatia miujiza na mambo ambayo ameendelea kufanya mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akiwa jimboni kwake na nje ya bunge kwa maslahi ya Taifa.

Wamezungumza hayo kwa nyakati tofauti jana walipokuwa wakizungumza na wananchi na viongozi mia moja kutoka Ludewa walipelekwa bungeni na mbunge Deo Filikunjombe kushuhudia bajeti ya serikali ya mwaka 2014/15 na baadaye kwenda jijini Dar es salaam kuhudhuria semina ya siku mbili kuhusu kuimarisha chama na uongozi.

Kwa upande wake Hilda Ngoye mbunge wa viti maalum Mkoa wa mbeya ambaye pia ni mzaliwa wa wilaya Ludewa amewaasa wanaLudewa kuacha kubadilibadili viongozi hususani wabunge kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kuendelea kurudisha maendeleo nyuma kwa sababu kila mbunge anahitaji muda ili kujipanga kwa sababu maendeleo hayaji kwa siku moja.

‘’’ wanaludewa napiga magoti mbele yenu mimi mtu mzima kuwasihi muwe na subira katika chaguzi kwani kuna viongozi wengine ni msaada katika maendeleo yetu lakini tunawapoteza kwa ajili ya tamaa zetu na kukosa msimamo kwa kudanganywa na watu wasio na manufaa kwetu.’’’ akasisitiza Ngoye

Ngoye aliwaonya watu wanaojipitisha kwenye jimbo la Ludewa na kumchafua Deo Filikunjombe kuwa wasiwadanganye wananchi badala yake wamuunge mkono mbunge wao ili kuleta maendeleo haraka kwa sababu jitihada zake zinaonekana wazi hakuna anachoshindwa.

MWISHO




No comments: