RIWAYA;MAMA YANGU MUUAJI
MTUNZI;Moringe john Mhagama
SEHEMU YA KWANZA
Kila mtu aliyefika pale
nyumbani alionekana kunishangaa kwa mwonekano
niliokuwanao,sikuonekana kabisa kushughulika na msiba ambao mimi
ndiye mfiwa pekee wa moja kwa moja niliyekuwepo pale.
Hakukuwa na ndugu
mwingine aliyekuwepo zaidi ya marafiki wa marehemu mama yangu ambaye
katika maisha yangu yote niliyoishi naye sikuwahi kuwaona ndugu zake
wengine hadi masaa machache kabla ya kifo chake ambapo aliniambia
ukweli si tuu ulimuumiza yeye bali hata mimi uliniumiza sana na
kufanya niamini kuwa mama yangu alikuwa muuaji ,kitendo ambacho sina
hakika kama mungu alimsamehe kwani hata kifo chake kilikuwa cha
kujiua.
‘’Yule kijana kama hajafiwa yaani
hana habari kabisa’’ilisikika sauti ya mama mmoja ambaye
alionekana kuumizwa na tabia niliyooneshwa.
‘’Huwezi jua mama ni mama anaweza
kuwa anaumia kwa ndani’’Alijibiwa na mama mwingine wakati huo
idadi ya watu ikizidi kuongezeka kwani marehemu mama yangu kabla ya
kifo chake alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa na marafiki wengi
nadhani kutokana na tabia yake ya kucheka na kila mtu aliyokuwa nayo
.
‘’Hapana huyu kijana amezidi
haiwezekani mtu umefiwa na mama yako mzazi halafu masaa yote unacheza
na simu yako tuu’’Alidakia mama mwingine ambaye kabla ya kifo cha
mama alikuwa akija mara kwa mara pale nyumbani.
‘’Labda anawasiliana
na ndugu zake awape taaarifa za msiba’’Ilisikika sauti nyingine
kwani kitendo change cha kuonekana nimevaa ‘earphones’ ziliwapa
uhuru wa kuongea kwa sauti ya juu wakiamini sikusikia chachote
ambacho walikiongea.
‘’Ana ndugu huyooo
mama yake hawajui si wa upande wa baba si wa upande wa mama’’Yule
mama aliyeanzisha majadiliano aliongea akionekana kuijua historia
yetu huku maneno yake yakinifanya niondoke mahali pale na kuingia
chumbani kwangu huku nikikumbuka yale aliyoniambia mama yangu
nikijaribu kuyapima kama yalikuwa na ukweli wowote.
Nilikumbuka kauli ya mama
kuwa aliamua kujiua kutokana na mambo kumwelemea na hatari iliyokuwa
mbele yake kukosa njia ya kujiokoa.Sikutaka kabisa kuamini kama
aliyoyaongea yalikuwa ya ukweli au kulikuwa na jambo lingine
lililojificha hadi kumpelekea mama yangu ndugu yangu wa pekee
niliyemfahamu hapa duniani.
Nakumbuka tofauti na siku
nyingine mama yangu alirudi mapema siku ile akiwa kwenye hali tofauti
na niliyomzoea siku zote kwani alikuwa na tabia ya kuingia pale
nyumbani kwa matani na vichekesho vya hapa na pale kila alipofika.
Siku ile baada ya kutupa
kibegi chake kochini alikaa chini na kuniomba nimpe chai jambo ambalo
nililifanya kwa haraka kwani haikuwa kawaida kwake kuwa vile hivyo
hali iliyonifanya niamini kuwa huenda alikuwa anaumwa.
‘’Mwanangu usiogope
haya ni maisha ya kawaida unaonekana kumwogopa mama yako usimwogope
leo ameamua kuwa mkali kama baba yako’’Aliongea mama yangu
akikoroga sukari kwenye chai aliyoimimina huku akijilazimisha
kutabasamu tabasamu ambalo lilishindwa kuishi usoni pake hata kwa
sekunde kumi na kicheko chake kikiishia kooni na kuniongezea hofu na
si kunitia tumaini tena. ‘’
Hapana mama utakuwa
unaumwa au kuna watu wamekuvuruga huko kazini kwako ‘’Niliongea
kwa masikitiko makubwa kwani mara nyingi ilikuwa kawaida kunieleza
jambo lililomkera huko kazini kwake. ‘’Hapana mwanangu nataka
nikuambie kitu kimoja muhimu sana ‘’Sauti yenye mikwaruzo
ilisikika na kunifanya nimsikilize kwa umakini mkubwa.
‘’Kama kitu muhimu
ndio uwe hivyo mama?’’Niliongea kwa hofu ambayo mama yangu
aliigundua na kujifanya kucheka kicheko ambacho ni kama kilikuwa na
ugonjwa kwani hakikuendana na hali niliyoiona usoni mwake. ‘’
Ndiyo najua hunifahamu
vizuri mwanangu nataka unijue mama yako nilivyo na sababu ya mimi leo
kuwa hivi maisha haya hayaeleweki naweza hata nikafa hata usijue
historia yako’’Aliongea mama yangu na kuchukua kikombe cha chai
kisha kunywa funda moja.
‘’Kwani si ulisha
niambia juu ya maisha yako mama kwa nini unapenda kukumbuka mambo
yakuumizayo tumepata nafasi ya kubaki hai basi tuendelee kuishi huku
kazi yako Mungu kakubariki kuifanya na inatufanya tuishi kwa hiyo
hakuna ulazima wa sisi kendelea kulalamika…..’
’Uchungu ulionishika
juu ya kumbukumbu ya maisha yetu zilinifanya nishindwe kabisa
kuvumilia na kujikuta naanza kulia bila kujua historia ya maisha yake
iliyo ya kweli ambayo kila nikiikumbuka inanifanya niseme’’ MAMA
YANGU MUUAJI’’.
*******
Machi 27 1994 RWANDA Chuki baina ya
makabila mawili makubwa nchini Rwanda ilizidi kuongezeka huku watu wa
kila kabila wakiamini kuwa wenzao kutoka kabila lingine ni watu
wabaya na wasiostahili kuishi jambo lililozidi kuchochea na kuongeza
mauaji yale.
Wahutu waliwaona Watutsi ni watu wabaya
kwao huku upande wa pili ukiamini kinyume chake na mauaji yakizidi
kuongezeka kila siku huku kila usiku ukiwa ni usiku wa mauaji ambako
watu wengi walikuwa wakipoteza maisha kwa mateso makubwa.
Umoja wa Mataifa na nchi nyingine
zilionekana kulalamikia tukio lile huku vyombo vya habari
vikihamishia kamera zao na wandishi wao kwenye nchi hiyo ndogo ambayo
ilikuwa kabla ya vita vya kwanza ya Dunia ilikuwa ni sehemu ya
Tanganyika.
pamoja na nchi jirani ya Burundi na
habari kufikia hata idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la
Uingereza(BBC) kuandaa kipindi maalum cha mambo yaliyoendelea nchini
humo wakiwahoji wanachi mbalimbali huku wakiongea na viongozi wa
Serikali ambao nao hisia zao za ukabila zikijionesha kila
walipohojiwa.
Wakati hayo yakiendelea katika kijiji
kimoja kilichokuwa Mashariki kabisa mwa nchi ile mtoto mmoja alikuwa
akitetemeka kwa hofu baada ya kushuhudia wazazi wake wakiuawa kinyama
kupitia kitundu kidogo kilichokuwa chooni kwani baada tu ya yeye
kuingia chooni watu wenye silaha za jadi waliivamia familia yake
iliyokuwa na wazazi wake na ndugu zake wawili wa kike na wakiume na
kuwaua kikatili
Alisubiri hadi wale watu walivyoondoka
na kuanza safari ya kutoroka kijiji kile huku akiwa hajui ni sehemu
ipi iliyokuwa salama kwake.Harufu ya damu za wazazi na ndugu zake
ilisikika kila alipokumbuka kilichomfanya atoe machozi kila wakati.
Safari isiyokuwa na mwongozaji ilipitia
katikati ya msitu mmoja ambao aliusikia katika hekaya za wazazi wake
kunwa ni msitu uliokuwa na maajabu mengi na lilikuwa ni jambo la
kawaida kupotea kwenye msitu huo.
Japokuwa alikuwa muoga lakini kitendo
cha kushuhudia vifo vya wazazi wake kilimwongezea nguvu ya kusonga
mbele akiepuka mauaji yale akiwa katikati ya msitu ule binti huyo
mwenye umri wa miaka mitano anazidiwa na njaa na kupoteza fahamu
kutokana na njaa aliyokuwa nayo.
Baada ya masaa matatu kuna sauti za
watu ambao walionekana kuwa makini kwa kila hatua
waliosogea,wakimvizia nyoka mmoja mkubwa ambaye walikuwa
wamemfuatilia kwa umbali wa zaidi ya kilometa kumi wakitaka kumuua
ili tuu wapate ngozi yake ambayo ilionekana wakiihitaji sana kwa
kipindi kile.
Hawakujua kabisa uelekeo
wa nyoka Yule ulikuwa ni kufuata chakula ambacho alihisi uwepo wake
mahali pale.Chakula hicho hakikuwa kingine zaidi ya mwili wa Yule
binti aliyeyaacha magofu yakiwa na mizoga ya watu waliouawa na
binadamu wenzao kisa kikiwa ni chuki tuu za ukabila japo kwa wakati
ule aliambiwa tuuwatu fulai ni wabaya lakini hakuwahi kufikiria kuwa
wanaweza kufikia hatua ya kuwaua ndugu zake.
Kwa kuwa jioni ilikuwa
imekaribia watu waliokuwa wakimwinda Yule nyoka ili tuu wamuangamize
ii wapate walichokitaka bila ya kuvunja masharti ya mganga wao
aliyewataka wampelekee ngozi ya nyoka huyo ambaye alikuwa hajatoka
kumla mtu ili dawa yao ifanye kazi vizuri na sharti gumu kabisa
lilikuwa ni kumuua Yule saa kumi na mbili na nusu jioni vinginevyo
wasingepata walichokitaka.
Lakini ghafla walishtuka baada ya
kumwona nyoka Yule akiongeza mwendo na kuwafanya wahisi kuwa huenda
aligungua kuwa alikuwa anafuatiliwa ama kuna chakula mbele yake kwani
nyoka huyo ilisemekana alikuwa akila nyama hasa za watu na hiyo ndiyo
sababu ya watu wengi kuuogopa msitu ule.
na mara chache alikuwa akivamia vijini
na pwani ya ziwa Tanganyika na kuwavamia wavuvi,Ilisemwa kuwa nyoka
huyo alikuwa ni mungu wa kabila Fulani nchini Burundi lakini makao
yake makuu yalikuwa ni katika msitu huo uliokuwa umepita kuanzia
Burundi hadi sehemu ya Rwanda.
Hatimaye nyoka Yule alikuwa hatua mbili
kabla ya kuufikia mwili wa msichana Delphine Daniel ambaye alikuwa
amepoteza fahamu huku sababu kubwa zikiwa ni njaa na uchovu wa safari
ya kutwa nzima
‘’Shiii……’’ilisikika
sauti iliyomshtua Yule nyoka wakati huo zilikuwa zimebaki dakika kama
kumi ufike muda walioambiwa na mganga wao kuwa walitakiwa kumuua Yule
nyoka na kumfanya Yule nyoka aachane na chakula kilichokuwa mbele
yake na kuwageukia maaadui wake ambao hakujua walimfuatilia kwa
takribani masaa matatu yaliyopita.
Mapambano ya mikuki na mishale kutoka
kwa watu watano waliokuja pale kwa lengo moja tuu la kumuua Yule
nyoka saa kumi na mbili na nusu.Lakini walitakiwa kumzuia tuu
asiwadhuru ili dakika kumi zilizobaki ndipo wammalize lakini sumu
kali alizozitema ziliwafanya wawili kati yao wapoteze uwezo wa kuona.
Mate ya sumu yalifika
moja kwa moja machoni mwao na wale wengine kupata muwasho
uliowapunguzia umakini kwani hawakujua kabisa kama mwenzao aliyewekwa
kwa ajili ya kuwasomea muda alikuwa amepoteza uwezo wake wa kuona
hivyo walipambana tuu akisubiri wakati ufike.
‘’Mhh muda
haujafika?’’Aliuliza mmoja wao huku akijikuna shingoni kwake
baada ya kutemewa mate yenye sumu na Yule mtu.
‘’Jamani
sioni’’Alijibu Yule msoma muda akijaribu kumpa saa Yule mwenzake
lakini kabla hata ya kuipokea ile saa aliona ile saa ikirushwa mbali
na mkono wake ukikoswa koswa na sumu iliyorushwa na Yule nyoka ambaye
tofauti na nyoka wengine alitumia sumu kumdhibiti adui yake kisha
kummeza akiwahai hivyo sumu ndiyo ilikuwa ikitumika sana katika
mapambano yake.
‘’Puuuh…..’’Ni
mlio uliosikika baada ya joka lile kuelemewa na mkuki mmoja uliokuwa
na sumu kali ulipita karibu kabisa na kinywa chake.‘’Poleni
jamani kwa hiyo hamuoni kabisa?’’Aliongea Yule aliyeurusha ule
mkuki akimsogelea Yule myoka mkubwa kabisa ambaye akipita sehemu ni
kama gari lilikuwa limepita.
‘’Ndiyo lakini si mbaya umasikini
kwa heri’’Aliongea mmoja kati ya wawili waliokuwa wamepoteza
uwezo wow a kuona akijikuna kalibu kabisa na jicho lake bado kazi
kubwa sana kumchuna ngozi yake ya tumbo na kufanikiwa kupita nayo
hadi kufika Ukerewe kwa mtaalamu’’Aliongea mwingine huku lafudhi
yake ya kihehe ikishindwa kujificha.
‘’Harafu yure ariyerara pale ni
nai’’Aliongea Mwita ambaye alikuwa ni kama kiongozi wao.
‘’Sasa we Mkurya unaniuliza mimi
wakati sioni si utani huu?’’Alisikika kijana mwingine
aliyeonekana ni kabila watani na wakurya ambaye licha ya kupoteza
uwezo wake wa kuona furaha yake ya kuukwepa umasikini ilimfanya
asijute kabisa kupatwa na tatizo lile.
‘’Ngoja tukamwone aliinuka Mwita
akiwaacha wenzake wakiendelea kumchuna Yule nyoka ngozi yake ya
tumboni.
Lakini kabla hata ya kumfikia Yule
binti mvua kubwa ilianza kunyesha eneo lile walilokuwa na hata
walipojaribu kutoka kuna nguvu ya ajabu iliwazuia kufanya hivyo.
‘’Haya maajabu mvua gani ituzunguke
sisi pekee?’’Alisikika kijana mwingine akiacha kufanya kazi ya
kumchuna Yule nyoka.
ITAENDELEA
Je,walifanikiwa kutoka na ile ngozi?
Kuna uhusiano gani na mama Muuaji na
hawa watu?
No comments:
Post a Comment