MANGULA AMWAGIA SIFA FILIKUNJOMBE KWA
KUTEKELEZA MIKAKATI YA CCM
Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara
Bw.Philipo Mangula amemwagia sifa mbunge wa jimbo la Ludewa mh.Deo
Filikunjombe kwa kuanza kutekeleza mipango mikakati ya chama cha
mapinduzi ambayo ililenga kutoa mafunzo kwa viongozi wa chama hicho
katika ngazi ya kata,vijiji na matawi ili kukiboresha chama katika
utendaji.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na
Bw.Mangula makao makuu ccm Dodoma alipotembelewa na mh.Filikunjombe
akiwa na viongozi wa ccm 92 kutoka wilayani Ludewa ambao
walisafirishwa na Mbunge wao kwalengo la kupata mafunzo mbalimbali
yahusuyo chama cha mapinduzi.
Bw.Mangula alisema Filikunjombe
amefanya kazi ambayo chama katika mipango yake kilipanga kufanya
hivyo ni mbunge wa mfano kwa chama kwani anafanya kazi ambayo
italeta manufaa makakubwa kwa chama hasa katika kipindi hiki
kinachokaribia uchaguzi wa Serikali za mitaa.
“Hongereni wanaccm wilaya ya Ludewa
kwani mmekuwa mfano wa kuigwa kwa wilaya nyingine nchini kupitia
mbunge wenu,hali hii si ya kawaida kutokana na ukweli kwamba chama
katika malengo yake tumesisitiza kila wilaya kufanya mafunzo kwa
viongozi wa kada zote ili kuweza kujihakikishia ushindi mwaka 2015
lakini nampokeza mbunge wenu Filikunjombe kwa kuanza na utekelezaji
wa agizo hilo na naomba wengine waige jambo hili”,alisema
Bw.Mangula.
Aidha mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe
Mh.Deo Sanga(Jaa people) amemuunga mkono Filikunjombe kwa kazi hiyo
ya chama ambapo alisema haijawahi tokea kuona mbunge akawasafirisha
viongozi wa chama chake kwa wingi kiasi hicho hadi Bungeni kwaajili
ya mafunzo hivyo huo ni ukomavu wa siasa na ni lengo zuri la
kukiboresha chama hasa katika ngazi za chini.
Mh.Sanga Jaa people alisema amejifunza
kitu kutoka kwa Filikunjombe hivyo hata yeye anapaswa kufanya hivyo
ili kuhakikisha chama cha mapinduzi katika jimbo lake kinasimama
imara kwani viongozi walio wengi katika ngazi za wilaya na kata hata
vijiji bado wanahitaji elimu ya kutosha katika kusimamia majukumu yao
ya kila siku.
Alisema katika maeneo mbalimbali
kumekuwa na tabia ya baadhi ya wabunge kufanya mambo hayo katika
ngazi ya wilaya na kuwasafirisha Madiwani katika kujifunza mambo
mbalimbali lakini Filikunjombe ameanza na viongozi wote wa kata za
wilaya ya Ludewa hivyo ni mfano wa kuigwa kwa wabunge wengine wa
chama cha mapinduzi hasa ndani ya mkoa wa Njombe.
“kwa kweli Filikunjombe amenifundisha
kitu mimi na wenzangu,hata siku moja sikuweza kufikilia kufanya jambo
kubwa kama hili na hakuna atakaye beza jambo jema ndani ya ccm kama
hili,ninachowaomba wajumbe mkaitumie elimu hii mlio ipata kwa mbunge
wenu ametumia fedha nyingi katika kuwasafirisha na kuwahudumia mpaka
mnaporudi hivyo msimuangushe yeye na chama cha mapinduzi katika
utekelezaji”, alisema Mh.Sanga Jaa people.
Wajumbe hao kutoka wilaya ya Ludewa
ambao ni wenyeviti wa ccm kata,makatibu kata na makatibu uenezi na
itikadi wa kata walifanya ziara hiyo ya mafunzo mjini Dodoma ambapo
walipata fulsa ya kuhudhuria kikao cha bajeti hasa kipindi cha
maswali na majibu katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment