MBUNGE
wa jimbo la Ludewa Mkoani Njombe kupitia chama cha mapinduzi (ccm)
Deo Filikunjombe amewahakikishia wananchi wanaoishi mwambao wa ziwa
nyasa kuwa atasherehekea pamoja nao sikukuu za X-Mass na mwaka mpya
kwa kutumia umeme.
Filikunjombe
aliyasema hayo jana alipokwenda kuzindua na kisha kushiriki nguvukazi
ya kufyeka njia ya umeme, kuchimba mashimo na kusimika nguzo hizo
kwa kushirikiana na wananchi wa kata ya Lupingu ambako mradi huo
umeanza baada ya serikali kutoa jumla ya shilingi bilioni 1.2 kati ya
shilingi b.1.3 zilizopangwa kukamilisha mradi huo.
Akizungumza
katika eneo la mradi Filikunjombe alisema tumeamua kufanya nguvu kazi
hii kwa wananchi wa vijiji vitatu vya Nindi, Lupingi na Mtumbati kwa
sababu kubwa mbili tumeshindwa kusubiri mpaka serikali itakapopata
fedha za kutosha mradi ambazo shilingi bilioni 1.3 lakini fedha
iliyopatikana ni bilioni 1.2 tu.
nikaambiwa
nisubiri fedha ikamilike ndipo nipewe kukamilisha mradi.
’’’ jumla
ya shilingi b.1.3 zilipangwa kukamilisha mradi huu wa umeme kutoka
Ludewa hadi Lupingu lakini serikali ikapata bilioni 1.2 ni kutokana
na hali hiyo nililazimika kuja kuzungumza na wananchi wangu ili
tuchangie nguvu kwa kusafisha njia, kuchimba mashimo, kusimika nguzo
na kuzisogeza.’’’
Wananchi
walifurahia na kuunga mkono jitihada za serikali za kuleta umeme
katika vijiji vilivyo pembezone mwa mwambao wa ziwa nyasa kwa
kujitolea nguvu zao ili kuokoa jumla ya shilingi milioni 100 ambazo
zingetolewa serikali kuwalipa vibarua.
Hii
ni nuru ya matumaini kama wananchi wangekataa na kusubiri serikali
tungekuwa bado tunasubiri lakini kwa kuwa umeme ni wao na manufaa ni
yao fedha zote zinztokz serikalini kupitia Tanesco.
Kuhusu
baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoshawishi wananchi wasishiriki wala
kujihusisha na shughuli za maendeleo yao Filikunjombe aliwataka
wanasiasa kuacha mawazo finyu na potofu serikali haiwezi kufanya kila
kitu watumie vema ridhaa waliyopewa na wananchi.
‘’’ nilipoingia
madarakani nilikuta mradi mmoja tu wa umeme kila mwananchi mwenye
macho anaweza kuona Ludewa tulikuwa nyuma, tumechelewa sasa
tunakwenda mbele walau nuru ya matumaini inaonekana nashukuru rais
kutuunga mkono barabara zinakwenda, miradi ya Liganga na Mchuchuma
inaendelea.’’ aliongeza mbunge
Aliongeza
kuwa wakati anaingia madarakani alikuta kijiji kimoja tu katika
vijiji 77 kikiwa na umeme lakini leo kuna vijiji 10 na sasa kuna
mpango kabambe wa kupeleka umeme katika vijiji 49 vilivyopo katika
kata za milimani na mwambao wa ziwa.
Filikunjmbe
amewataka viongozi kutengeneza mazingira mazuri ili kupunguza wimbi
kubwa na vijana na wananchi kukimbilia mijini ambako kuna huduma
nzuri Ludewa ni kubwa kuliko wilaya zote za mkoa wa njombe ina zaidi
ya skwea mita 8000 lakini tuna watu wachache kuliko wilaya zingine ni
kwa sababu ya vijana kukimbia.
No comments:
Post a Comment