Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

June 04, 2014

TAMASHA LA UMOJA KWANZA LAFANA WILAYANI LUDEWA



 WACHEZAJI WA TIMU YA UPLANDS FM RADIO WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WACHEZAJI WA TIMU YA LUDEWA FC SIKU YA TAMASHA LA UMOJA KWANZA.
 HII NI TIMU YA LUDEWA FC WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA
TIMU YA UPLANDS RADIO WACHEZAJI WAKE WAKIFANYA MAZOEZI KABLA YA KUINGIA UWANJANI

 LUDEWA FC WAKIFANYA MAZOEZI KABLA MCHEZO KUANZA
 ELMETHEW KIKA  WA UPANDE WA KUSHOTO NA WA KATIKATI AFISA HABARI MKOA WA NJOMBE ALIYEWAKILISHA MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI KATIKA KUUNGA MKONO JITIHANDA ZA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI NA WA KWANZA KUTOKA UPANDE WA KULIA NI MWAMUZI WA PAMBANO HILO BW.STEPHANO MAHUNDI WAKISUBIRI KUANZA KANDANDA DHIDI YA UPLANDS NA LUDEWA FC


 TIMU ZOTE MBILI UPLANDS NA LUDEWA FC WAKIPEANA MIKONO KABLA YA KUANZA MECHI
 WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA BONGOFRAVER KUTOKA WILAYA YA LUDEWA WAKIFANYA MAONESHO KATIKA UWANJA WA BURUDANI KWENYE TAMASHA LA UMOJA KWANZA LILILOANDALIWA NA RADIO UPLANDS FM KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI BINAFSI NA SERIKALI YA MKOA WA NJOMBE KUPIGA VITA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI.
WA PILI KUTOKA UPANDE WA KULIA NI AFISA HABARI MKOA WA NJOMBE CHRISTOPHA AMBAE AMEKWENDA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.

Timu ya Ludewa fc imefanikiwa kuichabanga goli nne kwa mbili dhidi ya Uplands fc katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Ludewa  mjini na kujinyakulia mbuzi aina ya beberu kwa ushindi huo.


Mbuzi huyo ambae aliandaliwa na  kampuni ya Uplands Radio kutoka Njombe mjini aliifanya timu ya Ludewa kuonesha kipaji chao katika kusakata kabumbu siku ya tamasha la Umoja kwanza lililoandaliwa na Uplands fm Radio kwa kushirikiana na serikali na taasisi mbalimbali.


Tamasha hilo lililenga kuhamasisha jamii kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI amba lilibeba ujumbe usemao Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI NI Zero Ambalo linatarajia kuendelea tena katika wilaya ya Makete mkoani Njombe juma mosi ya hiki hii .




 WANANCHI WILAYA YA LUDEWA WAKIWA KATIKA KUSHUHUDIA WASANII MBALIMBALI WAKITUMBUIZA KWENYE TAMASHA LA UMOJA KWANZA WILAYANI HUMO





 HUYU NI MC WA TAMASHA LA UMOJA KWANZA  MAMA NYEUPE JINA LAKE HALISI PILI NYENJE
BURUDANI KALI TOKA KWA WASANII WA KUNDI LA KIBENA ARTS GROUP WAKIBURUDISHA UMATI WA WANANCHI WALIOFIKA ENEO LA TUKIO WILAYANI LUDEWA AMBALO LILIBEBA UJUMBE WA MAAMBUKIZI YA VIRUSI NI ZERO

Uplands fm radio kutoka Mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na taasisi nyingene za binafsi na uongozi wa serikali  mkoa wa Njombe  imeandaa tamasha kubwa ambalo limelenga kuelimisha jamii mkoani humo juu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa kutembelea Wilaya zote za mkoa huo ambapo Jumamosi ya wiki iliyopita tamasha kubwa lilifanyika wilaya ya Ludewa.


Meneja wa kituo cha Radio Uplands fm Novatus Lyaluu amesema kuwa Tamasha hilo limeshilikisha wadau mbalimbali wakiwemo wadau  wa kupambana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Mkoa wa Njombe watu wa Kuhamasisha matumizi ya Kondom  PSI Na kwamba tamasha hilo linatarajia kuendelea tena jumamosi ya wiki hii wilayani Makete na baadae Wanging'ombe na Makambako kwa kila Juma mosi.

No comments: