Padre Ditrik Kayombo akiwa pamoja na mwandishi wa mtandao huu
wanafunzi wa shuo cha ufundi Lupanga wakiimba kwaya
Wanafunzi waliopata komunio ya kwanza kanisa katiriki Lupanga
Mtoto Nancy Isaack Makinda akijiandaa kula chakula baada ya kupata komunio ya kwanza
Mwanadaaji maarufu wa keki wilayani Ludewa Mama Mbena akimpa zawadi mtoto Nancy
Mama mzazi(mama Makinda)Nancy akimvisha taji mwanae
Nancy Makinda akiwa pamoja na dada zake pamoja na mdogo wake mara baada ya kupata Komunio ya kwanza
Nancy akikata keki
Nancy akilishwa keki
Familia nzima ya Isaack Makinda ikiwa katika picha ya pamoja
Paroko wa kanisa katoriki Lupanga
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe Ditrik Kayombo amewataka
waumini wa kanisa hilo nchini kuiheshimu Rozali kutokana na waumini
wengi katika miaka ya karibuni kurubuniwa na baadhi ya wahubiri na
kucha sala ya Rozali.
Paroko Kayombo aliyasema hayo jana
katika kanisa katoriki lililopo kijiji ja Lupanga wakati akiwapa
komuniyo ya kwanza wanafunzi wa shule ya msingi ya St.Mamalio Lupanga
ambayo inamiaka mitatu tokea shule hiyo ianzishwe.
Alisema imefika wakati wakatoriki
wanatakiwa kubaki katika misimamo yao hasa katika sala ya Rozali
ambayo imekuwa ikitumiwa na waasisi wa kanisa hilo katika kumkumbuka
Yesu Kristo na mama yake Maria kila mara.
“Nawaomba wazazi wa watoto hawa
mkawaendeleze kwa kusali nao mara kwa mara sala ya Rozali kwani
imekuwa kawaida ya baadhi ya wazazi kupuuza baadhi ya sala hali
ambayo haipendezi katika misingi ya katoliki”,alisema Paroko
Kayombo.
Alisema kuwekuwa na baadhi ya
wachungaji wa madhehebu mengine ambao huwakatisha tamaa kwa kutoa
lugha za kejeli kwa kuwazuia kutosali sala ya Rozali wakiwa na
kisingizio cha kuwa wanamuabudu bikila Maria hali ambayo si kweli.
Paroko Kayombo aliwasihi watoto hao
kutozisahau rozali zao alizowavisha ili kujikumbusha mara kwa mara
katika sala hiyo ambayo itakuwa kama tamaduni kwa watoto hao ambao
walipata komuniyo ya kwanza kijijini Lupanga.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment