Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

June 13, 2014

WABUNGE WA CCM NA UPINZANI WAWATAKA WANALUDEWA KUBAKI NJIA KUU.

wajumbe wa ccm kutoka Ludewa wakilivuta basi walilosafilia kuelekea bungeni Dodoma ambalo lilikwama katika tope mlima wa Jongojongo wilayani humo.


wenyeviti wa ccm wa kata za wilaya ya Ludewa wakiwa katika picha ya pamoja
makatibu waenezi wa ccma kata za Ludewa wakiwa katika picha ya pamoja

Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ludewa Stanley Kolima akisalimiana na Mh.Kawawa katika viwanja vya Bunge
Waziri mkuu Mh.Pinda akiwa na Deo Filikunjombe akiwasalimia wajumbe wa wilaya ya Ludewa katika viwanja vya Bunge
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wao Filikunjombe katika viwanja vya bunge

 Filikunjombe akiwa na Kapteni Komba

Makatibu wa ccm kata za Ludewa wakiwa katika picha ya pamoja





kapten Komba akiongea na wajumbe
Makamu mwenyekiti wa ccm Taifa Bw.Philipo Mangula akiongea na wajumbe
wajumbe wakiwa bungeni
Filikunjombe akitoka na wajumbe bungeni
waandishi kutoka Ludewa akiwa na Filikunjombe katika viwanja vya bunge




Wabunge wa chama cha mapinduzi(CCM) na wale wa upinzani wamewataka wananchi wa wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe kubaki njia kuu kwa kuendelea kubaki na Deo Filikunjombe katika uchakuzi ujao na kuacha tabia iliyozoeleka wilayani hapo ya kubadirisha wabunge kila kipindi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na wabunge hao katika hoteli ya kimataifa ya St.Gaspar iliyoko mjini Dodoma ambao walishiriki chakula cha jioni na viongozi 100 wa chama cha mapinduzi kutoka kata 25 za wilaya ya Ludewa waliosafirishwa na Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa lengo la kushiriki bunge la katiba na kupata mafunzo mbalimbali ya utawala.

Baadhi ya wabunge walioshiriki katika chakula hicho ni pamoja na Hilda Ngoye mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya ccm,Rita Kabati Iringa viti maalumu ccm,Gaudens Kayombo wa Mbinga na Kapten John Komba wa Nyasa,mwingine ni Kangi Lugola wa Mwibala,hao ni baadhi ya wambunge.

Wakiongea kwa Nyakati tofauti Mbunge wa wilaya ya Nyasa kapten John Komba lisema ni muda mrefu mikoa ya kusini imekuwa nyuma kwa maendeleo lakini kutokana na kupata wabunge makini ambao ni wasemaji bungeni na wanauchungu na wapigakura wao Serikali imesikia kilio chao na tayari maendeleo yameanza kuonekana.

Kapten Komba alisema wilaya ya Ludewa inasifika kwa kubadirisha wabunge kwa kila kipindi hali ambayo imesababisha kutokuwa na maendeleo kutokana na viongozi hao kuwa na mipango mizuri lakini kabla ya kutimiza mipango hiyo hutolewa madarakani.,

“Nawaomba wanaludewa muache tabia hiyo ya kuwabadili wabunge kama nguo,mmekuwa nyuma kwa miaka mingi katika maendeleo lakini hili jembe mlilolipata sasa msilipoteze kwa kudanganywa na wapenda madaraka ambao hawatawaletea maendeleo”,alisema John Komba.

Aidha Mh.Hilda Ngoye ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Nsisi kata ya Lifuma wilayani Ludewa aliwasihi wajumbe hao kwa kupiga magoti akisema imefika wakati wilaya ya Ludewa inatakiwa kuwa na mtu mpenda maendeleoa ambaye si mwingine bali ni Deo Filikunjombe.

Mh.Ngoye alisema ni miaka mingi kata za mwambao wa ziwa nyasa zimekuwa zikipata shida kubwa ya mawasiliano na Barabara hali iliyosababisha wananchi wengi hasa akina mama wajawazito kutembea kwa miguu kwa zaidi ya kilometa 45 kwa kufuata huduma za Afya lakini kwa sasa mambo yameanza kubadirika na wanaludewa kufaidi matunda ya uhuru.

Alitolea mfano barabara ya Ludewa Lupingu ambayo ilikuwa tatizo na kusababisha ajali mbaya kutokana na ukubwa wa safu ya milima Living stone lakini kipindi ambacho Filikunjombe ameingia madarakani ameweza kuishawishi Serikali na barabara hiyo umepata fedha za upanuzi na kuingizwa katika mpango wa Tanroad.

Mh.Ngoye alisema hiyo ni fahari kubwa na nikitu cha kujivunia kuwa na mbunge mwenye mawazo mazuri ambaye anawajali wananchi wake hivyo hakuna sababu ya kuhangaika zaidi ya kubaki njia kuu na kuepuka michepuko ya kutafuta kiongozi mingine.

Naye Mh.Deo Filikunjombe aliwataka wajumbe hao kutoka Ludewa wajifunze mazuri wanayoyaona na si vinginevyo hata hivyo alisema kuwa lengo la kuandika maneno ya baki njia kuu acha michepuko katika flana alizowagawia wajumbe hao ni kuwataka kubaki na CCM na kuacha kuhangaika na vyama vya upinzani tofauti na wengine wanavyotafsiri.

Ziara hiyo ya mafunzo kwa wajumbe kutoka Ludewa inatarajia kumalizika tarehe 16 juni mwaka huu ambapo baada ya kutoka Dodoma watasafiri kuelekea jijini Dar es Salaam kwaajili ya mafunzo ya kukiboresha chama yaani kuwaandaa vijana kuwa viongozi na wabaki ndani ya ccm na walioko nje warudi ccm jambo jingine ni pamoja na mafunzo ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mwisho.


No comments: