Hizi ni Baadhi ya vipodozi na dawa ailizozuiliwa na TFDA
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka mikoa 6 ya Nyanda za Juu Kusini wakiwa katika semina ya siku moja ya TFDA |
Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kanda Rodney Alananga akifafanua jambo wakati wa semina iliyowahusisha wanahabari 120 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. |
Mamlaka ya chakula na dawa nchini imeweka mkakati wa kukutana na nchi jirani ili kujadiri namna ya kudhibiti uuzwaji wa vyakula,dawa na vipidozi visivyo kidhi viwando ambavyo ni hatari kwa afya ya binadamu.
Akizungumzia suala hili leo katika semina ya siku moja katika ukumbi wa hospiatari ya mkoa wa Mbeya iliyowakutanisha waandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo vy habari Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo Bi.Charys Ugullum alisema kumekuwa na changamoto kubwa ya udhibiti kutokana na nchi jirani kutokuwa na sheria ya udhibiti wa bidhaa zisizo na viwango.
Bi.Charys alisema Tanzania inafanya kazi kubwa ya udhibiti ili kuhakikisha wananchi wake wanakula na kutumia dawa zilizo na viwango vya kimataifa lakini nchi jirani hazina sera za udhibiti hivyo imekuwa ni kazi ngumu kudhibiti mipakani ambako bidhaa hizo huingizwa kwa njia za panya.
"Kupitia waandishi wa habari ni matumaini yangu jamii itahamasika kutotumia vipodozi,vyakula na dawa zisizothibitishwa na TFDA kwani baadhi ya watanzania wamekuwa ni chanzo cha uingizaji wa bidhaa zilizotengenezwa chini ya kiwango na zenye kemikali nyingi ambazo ni hatari kwa afya ya binadamu",alisema Bi.Charys.
Aidha Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Kanda ya Mashariki Bwana Emmanuel Alfonce Amesema Kuwa Kwa Mujibu wa Takwimu za WHO kwa mwaka 2006 Zimeeleza Kuwa Tanzania Imekuwa na Asilimia kumi ya Biashara ya Dawa Duniani kwa Hasara ya Dola za kimarekani bilioni 500 Kutokana na Madawa Feki.
Bwana Alfonce Amesema Kuwa Baadhi ya watanzania wasio waaminifu wamekuwa wakijishughulisha na utengenezaji wa madawa feki kama vipodozi pamoja na madawa ya Hospitali kitu kinachosababisha madhara makuwa kwa walaji.
Aidha Mamlaka Hiyo ya TFDA Imewataka wanahabari Kuendelea Kusema Ukweli juu ya Vyakula Madawa Feki ambayo yamekuwa Yakiendelea Kusambazwa Kwa Wananchi Ili Kulinda Afya za Walaji.
Kauli Hiyo Imetolewa na Mwanasheria wa Mamlaka Hiyo Bwana Iskari Fute Wakati Akitoa Semina ya Siku moja kwa Wahariri na Waandishi wa Habari wa Nyanda za Juu Kusini Iliyofanyika Jijini Mbeya.
Awali akifungua Semina hiyo Kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya,Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Bwana Leonard Magacha Amesema Kuwa Kutokana na Jamii Kuamini Kila Kinachotangazwa na Vyombo vya Habari Hivyo Wanahabari Hawanabudi Kufanya Uchunguzi wa Kina na Kubaini Ukweli wa Kila Habari Kabla ya Kuitangaza.
Hata hivyo Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Imefanikiwa Kufungua Ofisi Nyingine Tano Katika Mikoa Tofauti Pamoja na Kufungua Maabara Kubwa yenye Kiwango cha Kimataifa Kwa ajili ya Kusogeza huduma karibu na Wananchi badala ya kubaki Dar es salaam.
Amesema matarajio ni kuendelea kusimamia Viwango vya ubora wa bidhaa,kuwaelimisha wananchi kupitia waandishi wa Habari hapa Nchini.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa usalama wa chakula bwana Justin Makisi amesema kuwa endapo mamlaka hiyo haitosimama vizuri katika kudhibiti matangazo ya biashara ambazo si halali na hazina ubora basi jamii itapata madhara makubwa na hata kusababisha vifo kutokana na kutumia madawa na vyakula vilivyokwisha muda wake.
Amesema kuwa kama mamlaka tayari imefanikiwa kupiga marufuku na kuyafungia baadhi ya matangazo yaliyoonekana kupotosha umma ikiwemo dawa ya asili ya Fiterawa inayodaiwa kutibu ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
Katika hatua nyingine amevitaka vyombo vya habari kutumia nguvu kubwa katika kuendelea kutoa habari na matangazo yanayopotosha umma katika maeneo mbalimbali ili jamii iweze kufahamu na kuepukana nayo.
Akizungumzia juu ya kushuka kwa ubora wa vyakula na Dawa mkurugenzi mkuu wa Maabara Bi.Charys Ugullum amesema kuwa kama maabara imekuwa ikifanya uchunguzi wa chakula,dawa na vidozi ili kubaini ubora na usalama wa bidhaa husika ili ziweze kuingizwa sokoni.
Ameongeza kuwa uchunguzi huo ukishafanyika unasaidia katika utoaji wa maamuzi juu ya chakula,dawa na vipodozi ambavyo vitabainika kuwa vina ubora au havina.
Amesema jumla ya sampuli 7546 za vyakula zimeshafanyika pamoja na vipodozi tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo mnamo mwaka 2003.
No comments:
Post a Comment