Na Ibrahim Yassin,Chunya
WANANCHI Wilayani chunya Mkoani
Mbeya wameiomba serikali kuanzisha huduma ya macho na mionzi katika Hospitali
ya wilaya ya chunya ili kupunguza gharama za kusafiri hadi hospitali ya Mkoa
Mbeya.
Wakizungumza na waandishi wa habari
Wilayani humo kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema kuwa hospitali ya
Wilaya hiyo haina kitengo cha macho na mionzi hivyo kupelekea wananchi
kusafiri umbali mrefu hadi kufikia hospitali ya mkoa au ya rufaa jijini mbeya.
Mkazi wa Kibaoni Obadia Mwaipopo
alisema kuwa wananchi wengi wilayani humo wanakabiliwa na matatizo ya macho
kutokana na matumizi holela ya dawa za kuchenjulia dhahabu maarufu kama
Mercury.
Mwaipopo alisema vijana kwa wazee
wanamatatizo ya macho hasa wale ambao wanashinda kwenye machimbo ya dhahabu na
hawana muda wa kuweza kuachia muda kwenda kucheki macho yao.
Aidha alisema kuwa iwapo serikali
itaanzisha kitengo cha macho na mionzi katika hospitali hiyo kutahamasisha
vijana na wazee kuweza kupima afya zao ikiwa ni pamoja na macho na magonjwa
mengine.
Naye Mama mmoja ambaye hakutaka
kutaja jina lake alisema kuwa akina mama na vijana wanama tataizo ya macho
kutokana na kutumia muda mwingi kwenye kuchekecha mchanga wa dhahabu wenye
vumbi kwenye makalasha.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa
hospitali ya wilaya Wilson Sichalwe alikili kutokuwepo kwa kitengo cha macho na
miyonzi katika hospitali hiyo na kusema kuwa ni jambo ambalo linapaswa
kupiganiwa ili kuokoa masha ya wanachunya na wengine.
Sichalwe alisema kuwa kitengo hicho
ni muhimu sana kwa wilaya hiyo kutokana na asilimia kubwa ya vijana na akina
mama ni watu wanaoshinda kwenye machimbo.
Alisema kuwa wakazi wengi wilayani
humo hawana muda kwena jijini mbeya kwa ajili ya kupima macho na huduma zingine
ambazo hazipo katika hospitalini hapo kutokana na wengi kushinda kwenye
makalasha ya dhahabu.
Ameongeza kuwa iwapo serikali
itafanikisha kuwepo kwa wataalamu hao kutarahisisha wananchi kutoka kambi
katoto na kwingineko kwenye umbali wa zaidi ya kilomita 200 kupata huduma ya
macho.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment