May 03, 2014
MADIWANI LUDEWA WAMKANGANYA MKURUGENZI, LAKINI AWANYAMAZISHA KWA KANUNI.
MADIWANI katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe wameshindwa kutunisha misuri kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo baada ya kulazimisha na kudai bila mafanikio mambo yaliyo juu ya uwezo huku wengi wao wakiwa mbumbumbu juu ya sheria na kanuni zinazoendesha halmashauri.
Hayo yalijitokeza katika balaza kuu la madiwani la robo ya pili ya mwaka lililofanyika Aprili 12 mwaka huu katika ukumbi wa halmashauri ambapo pamoja na mambo mengine madiwani hao walimlalamikia mkurugenzi wao Waziri kwa tabia ya kupuuzia maagizo mengi ikiwemo kutotekeleza agizo lao la kumtaka atafute fedha mahali popote kwa ajili ya ziara ya kujifunza katika maeneo yenye madini nchini kama vile Bulyankhulu na kwingineko.
Aidha hali ya hewa ilianza kuchafuka zaidi baada ya balaza hilo kumwagiza tena mkurugenzi huyo kutafuta fedha mahali popote kwa ajili ya kuwapeleka baadhi ya madiwani na wataalamu kwenda kukagua barabara ya Amani hadi Ibumi waliyodai kutengenezwa na mkandarasi chini kiwango.
Ni kutokana na agizo hilo ndipo madiwani walionesha udhaifu na uelewa mdogo wa mambo ikiwemo usahaulifu unaotokana na ukosefu wa umakini na kutokujali maslahi ya halmashauri yao hasa katika utoaji maamuzi yasiyo ya msingi bila kujali uwezo na pato la halmashauri yao.
Hata hivyo madiwani wachache wenye uelewa walionekana kukubali matokeo huku wengine wakibaki bila kuonesha msimamo wao baada ya kugundulika kuwa maagizo kama hayo yalikwisha kutolewa katika kamati ya uchumi, mipango na fedha, kwa hiyo agizo la balaza lilikuwa la pili yaani agizo juu ya agizo jambo lililomchanganya na kumshangaza mkurugenzi na kushindwa atekeleza agizo gani kati ya hayo mawili.
Akijibu na kutoa ufafanuzi wa maagizo ya madiwani hao mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa William Waziri alisema agizo kama hilo lilikwishatolewa na kamati ya uchumi mipango na fedha kwa kuagiza kuwa ni madiwani wawili tu wa kata ya Ibumi na kata ya Mundindi ambako barabara hiyo inajengwa.
“”” waheshimiwa madiwani nashindwa kuelewa nitekeleze agizo gani maana kamati ya uchumi mipango na fedha iliagiza kitu kingine na balaza limeagiza kitu tofauti hata hivyo wakienda madiwani na wataalam kukagua hakutakuwa na ufanisi ni vema wakahusika madiwani wa kata zinazoguswa na mradi huo ili kupunguza gharama.’’’’’ alisisitiza Waziri
Kufuatia mvutano huo ndipo mwanasheria wa Halmashauri ya ya wilaya ya Ludewa Nathani akaomba mwongozo wa mwenyekiti na kusoma kanuni namba 45 inayoelekeza uundwaji wa kamati ndogo na madaraka yake ambapo kanuni hiyo inaeleza wazi kwamba kamati ukishatoa maelekezo balaza haliwezi kutengua mpaka iamuriwe vinginevyo
Agizo lingine lililoleta utata na kuwa ngumu kutekelezeka ni lile na madiwani kumtaka mkurugenzi huyo kumwita kwa barua katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini kuja kutoa elimu na ufafanuzi kuhusu kushindwa kutekeleza agizo la rais la kufungua ofisi ya madini wilayani Ludewa baada kumwita kamishna wa madini kanda ya nyanda za juu kuhudhuria balaza bila mafanikio.
Maagizo kuhusu matumizi ya fedha yanatolewa na madiwani hao yamekuwa yakitolewa bila kuangalia uwezo wa halmashauri yao ingawa mkurugenzi huyo amekuwa akikubali nakuahidi kuyafanyia kazi kila anachoagizwa.
Halmashauri inategemea vyanzo vichache sana vya mapato ya ndani hata hivyo inapata fedha kidogo sana kutoka serikali kuu na fedha za uendeshaji halmashauri ni zaidi ya miezi miwili hazijaletwa jambo linalopelekea hata vikao vya madiwani kushindwa kufanyika kwa wakati pamoja na halmashauri kuidai bila mafanikioNFRA jumla ya shilingi m.400.
mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment