Katibu wa mbunge Filikunjombe Bw.Stanley Gowele akikabidhi kinanda
Bw.Gowele akikabidhi Genereta
Wananchi wa wilaya ya Ludewa wameendelea kunufaika na ahadi za mbunge wao Mh.Deo Filikunjombe kutokana na maeneo mengi kupewa vifaa na fedha ambazo aliahidi wakati akiomba ridhaa ya uongozi kwa wananchi hao.
Akikabidhi moja ya ahadi hivi karibuni katika Kanisa Katoliki Mlangali wilayani humo katibu wa Mbunge huyo Bw.Stanley Gowele alisema lengo la Filikunjombe ni kuona anakamilisha ahadi zote alizoziahidi kwa wananchi wake kabla ya mwaka 2015.
Akikabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni mbili,kinanda kimoja na jenereta moja kwa kwaya ya kanisa hilo Bw.Gowele alisema katika meeneo mengi aliyoahidi Filikunjombe tayari ameshakamilisha ahadi zake hivyo kinachotakiwa ni kumuombea ili aendelee kukamilisha maeneo yaliyobakia.
“Ahadi alizoziahidi Filikunjombe zinakaribia kukamilika katika jimbo lake lakini anachowaomba ni matumizi sahihi ya vifaa na fedha anazotoa ili kuleta manufaa katika kizazi hiki na kizazi kijacho bila ya kujali itikadi za vyama vya siasa kwani yeye ni mbunge wa wananchi wote wa Ludewa”,alisema Gowele.
Aidha Paroko wa kanisa hilo Baba Volka alimshukuru Filikunjombe kwa kutoa vifaa hivyo kutokana na kanisa la Mlangali kutokuwa na kinanda kwa muda mrefu hali iliyopelekea waumini kuchangishwa michango ili kuweza kununua.
Baba Volka aliwataka watu wengine wenye mapenzi mema na kanisa kuiga mfano kwa Filikunjombe kwa kujitolea kwani miaka ya nyuma kulikua na wafadhiri ambao walikuwa wakilisaidia kanisa lakini kwa sasa hakuna tena hivyo kinachotakiwa ni kuwa na moyo wa kujitolea.
Alimsifu Filikunjombe kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa michango yake mbalimbali kwa wananchi kutokana na hivi karibuni kufanya harambee iliyopelekea kufanikisha kiasi cha shilingi 35 milioni aliyo itoa yeye na rafiki zake katika kufanikisha ununuzi wa gari ya parokia ya Ludewa mjini.
Naye mzee maarufu katika kata ya Mlangali anayefahamika kwa jina la Mstaarabu aliwataka wanaludewa wenye nafasi mbalimbali walioko mijini kuoga mfano wa Filikunjombe katika kuiendeleza wilaya ya Ludewa.
Mzee Mstaarabu alisema baadhi ya vijana wanaotoka wilaya ya Ludewa wanapopata mafanikio wamekuwa wakisahau walikotoka na kulowea mijini hali mbayo inafanya wilaya hiyo kuwa nyuma kimaendeleo kutokana na vijana hao kutoshiriki katika ujenzi wa wilaya yao.
“Inashangaza kuona vijana tunao wasomesha wakishapata mafanikio wanapotelea mijini na kusahau walikotoka na wakati mwingine husahau hata kujenga nyumba ya kufikia wanapopata matatizo kama ya misiba hali ambayo inatia uchungu kwa baadhi ya wazazi,ninachowaomba vijana wetu kuiga mfano wa mwenzao Filikunjombe anayekumbuka kwake bila kujali kabila”,alilalamika Mzee Mstaarabu.
Aliseama Filikunjombe kabla ya kupata nafasi hiyo ya ubunge alikuwa akishiriki kikamilifu katika maendeleo ya wilaya yake ndio maana hata mtoto mdogo anamfahamu hivyo kinachotakiwa ni kumfanyia ibada maalumu ya kumjalia afya njema katika kazi zake.
Mwisho.
KWA UDHAMINI WA OTEWAS GUEST HOUSE AND BAR
WANAPATIKANA LUDEWA MJINI BARABARA IENDAYO POSTA
KWA MALAZI BORA NA ULINZI WA VIFAA VYAKO NENDA OTEWAS GUEST HOUSE
WAWEZA KUWASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0753464920/0769113759
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment