Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

April 08, 2014

WUTU WAWILI WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI.

WATU wawili ambao ni Mashaka Mrisho (22) na Ramadhani Singo (30) wakazi wa Kitongoji cha Kyela Kati Wilayani Kyela Mkoani Mbeya wamekamatwa na Polisi leo (jana)wakituhumiwa kuvunja maduka mawili na kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 100,

Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu katika eneo la tukio mwenyekiti wa kitongoji cha kyele kati Rameck Mbembela alisema kuwa watu hao wamevunja duka la M,pesa mali ya Willy Kalonga na kuiba fedha taslim Tsh,mil 2 na Tsh,mil,1 iliyokuwa kwenye simu voda com Tsh,laki 3 iliyokuwa kwenye Aiter money Tsh,laki 4 iliyokuwa kwenye Tigo pesa pamoja na pisi 60 za simu zenye thamani ya zaidi ya mil,3.

Mbembela alisema kuwa kijana mungine aliyevunjiwa na kuibiwa ni Yusuph Mazara ambaye aliibiwa vitu vya vyote vilivyokuwemo dukani humo pamoja na fedha suiliva zilizokuwa zimejaa bakuli huku akivitaja baadhi ya vitu kuwa ni katoni za sabuni,mafuta ya kula nay a kupakaa,simu pamoja na vitu vingine kadhaa ambavyo thamani yake bado haijajurikana.

Alisema kuwa kuibiwa kwa watu hao taarifa zilifika ofisini kwake na yeye kupeleka taarifa kituo kikubwa cha polisi ambao nao walianza msako na kufanikiwa kumkamata kijana aliyejulikana kwa jina la mashaka na ndipo walipoenda kupekuwa katika nyumba anayoishi na kukuta bidhaa hizo zikiwa zimehifadhiwa katika nyumba hiyo.

Alivitaja vitu hivyo vilivyokutwa kuwa ni Baiskel 19 aina ya kamango baiskel 4 kubwa,katoni za sabuni,mafuta ya kupikia, cement mifuko 16,malumalu dazeni 12,vipisi vya nondo 86,Tv 1,redio sabufa 1 katoni  2 za sukali juice katoni 1 sigara katon 2 pamoja na vitu vingine ambavyo vilichukuliwa na jeshi polisi na thamani yake bado haijajulikana.

Yusuph Mazara mmoja wa waliovunjiwa na kuibiwa alisema kuwa watu hao kabla ya kutenda tukio hilo walimteka mlinzi na kumpa kipigo kizito na kufanikiwa kuvunja na kuiba mali hizo na kuwa yeye hana tatizo na wezi hao isipokuwa anahitaji mali zake zirudi.

Naye Willy Kalonga mmoja kati ya watu walioibiwa kwa upande wake alidai kuwa amesikitishwa na kitendo hicho kwani yeye aliacha mauzo pamoja na vitu vingine dukani humo na kwamba kitendo cha kuibiwa kimempa wakati mgumu na kwa kuwa tayari wahusika wapo chini ya ulinzi anaiachia polisi ifanye kazi yake.
MWISHO
 
 Na Ibrahim Yassin,Kyela

No comments: