WATUHUMIWA
sita wa wizi wa kutumia siraha ambao ni Mashaka Juma(30) mkazi wa kyela
kati,Issa Israel (gwalugwaja)(35) mkazi wa ndandalo,Juma Julius(mbwa
mwitu)(31)mkazi wa Kajunjumele,Asedy Daud (41)mkazi wa bondeni,Musolini Mwamasinga
(34) mkazi wa bondeni na Hasani Shindo (31) mkazi wa Kyela kati wamefikishwa katika
mahakama ya wilaya ya Kyela mkoani Mbeya jana kujibu mashitaka yao
yanayowakabili.
Kwa mujibu
wa mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo Nickolaus Tbba ni kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa
na kesi tatu ya kwanza ni kuvunja nyumba kifungu cha 384 sura ya 16 ya kanuni
ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,kesi ya pili ni kuvunja nyumba na
kuibakifungu cha 296 na kifungu cha 265 sura ya 16 ya kanuni ya adhabu na kesi
ya tatu ni wizi wa kutumia siraha kifungu cha 287 A sura ya 16 ya kanuni ya
adhabu.
Tbba alisema
kuwa watuhumiwa hao walivunja na kuiba duka la Happy Kakusya na kuiba vitu
mbalimbali vyenye thamani ya Tsh,million 1,duka lingine walilovunja ni la Pipi
Yusuph ambapo watuhumiwa ni Mashaka Juma na Hasan Shindo na kuiba mali yenye Thamani
ya Tsh,2,90,000 na kuwa vitendo hivyo vilifanyika tarehe 27 na 29 mwezi huu.
Aliitaja
kesi ya tatu kuwa ni ya wizi wa kutumia silaha inayowahusu watuhumuwa sita kuwa
kabla ya kuvunja na kuiba pesa Tsh,Mil, 1,pisi 60 za simu zenye thamani thamani
ya Tsh,mil,2,na vitu vingine ambavyo jumla yake ni Tsh,Mil,5 na elfu 40,000
ambapo walimpiga na kumjeruhi na nondo kichwani mlinzi wa duka hilo Adam
Mwankuga.
Katika
tuhuma hizo washitakiwa wote waliyakana mashitaka hayo na wamerudishwa lumande
hadi tarehe 16 mwezi huu kesi yao itakapotajwa tena chini ya Hakimu mkazi
mfawidhi wa mahakama ya wilaya Joseph Luambano.
Katika hatua
nyingine Silvestar Mele (17) mkazi wa kitongoji cha Itunge wilayani hapa
amefikishwa mahakamani akituhumiwa kumchoma kisi hadi utumbo kutoka nje Gwamaka
mwamafupa siku ya tarehe 29 mwezi wa huu ambapo anashitakiwa kwa kifungu cha
225 sura ya16 ya kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka
2002,mshitakiwa amekana shitaka na amerudishwa lumande hadi tarehe 16 mwezi huu
kesi yake itakapotajwa tena.
Denis
Mwaipaja (20)mkazi wa Kitongoji cha mikoroshoni amefikishwa katika mahakama
hiyo kujibu tuhuma ya shambulio la haibu linalomkabili la kumkamata mwanamke na
kumtomasa tomasa katika sehemu za mwili wake bila ridhaa yake siku ya tarehe 29
mwezi huu na ameshitakiwa kwa kifungu cha 1435 kifungu kidogo cha (1) na (2)
sura ya 16 ya kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 na amekana
shitaka na yupo lumande baada ya kukosa mdhamini kesi itatajwa tena tarehe 16
mwezi huu.
Mwisho.
Na Ibrahim
Yassin,Kyela
No comments:
Post a Comment