Mtoto Frola Nsubili katikati akipokea msaada wa baiskeli
Na
Ibrahim Yassin,Kyela
SHIRIKA la
The Struggle for Community Support Alliance (SCSA) yenye makao makuu yake
wilayani Kyela mkoani Mbeya limetoa baiskeli moja aina ya kamongo yenye thamani
ya shilingi 120,000 kwa mtoto yatima aliyefanyiwa ukatili Frola Nsubili (13)
mkazi wa kitongoji cha Mbasi kijiji cha Lugombo Kata ya Mwaya wilayani hapa.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi msaada huo Naibu Katibu mkuu wa shirika hili Taifa
Alfred Mwansasu alisema kuwa walisikia tanzgazo la uwepo wa tatizo la yatima huyo
kwenye kituo cha redio Kyela nayeye kama Katibu aliwasiliana na mwenyekiti wa
shirika hilo kitaifa aliyekuwa Korea kusini kikazi ambaye alituma pesa hizo kwa ajili
ya ununuzi wa baiskeli hiyo pamoja na mambo mengine.
Akizungumza kwa
njia ya simu kutoka korea kusini mwenyekiti mtendaji wa shirika hilo kitaifa
Abraham Mwanyamaki alisema shirika lake limetoa msaada huo ili kumuwezesha
mwanafunzi huyo kwenda shule kirahisi na kwamba wataendelea kutoa misaada kama
hiyo pale watakapo hitajika kufanya hivyo.
Alisema pindi
atakaporejea nchini ataitembelea familia hiyo ili kujua matatizo mengine yanayo
ikabili familia hiyo na kuyatatua ikiwa ni pamoja na kutengeneza na kuboresha
makazi ya familia hiyo ili kuiwezesha
kupata furaha na kuwaondolea hudhuni waliyonayo.
Msichana
huyo ambaye hana wazazi wote wawili na anaishi na Bibi yake ambaye ni mremavu
alihitimu darasa la saba mwaka jana na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato
cha kwanza mwaka huu katika shule ya mwaya ambapo bibi yake alikusanya fedha
kidogo kutoka katika shughuri zake zan kilimo kwa ajili ya kumlipia karo lakini
kuna kikundi kilichodaiwa kuwa kimepewa mamlaka na halmashauri kuwalipisha watu
wanaolima kando ya ziwa nyasa.
Akizungumza
kwa masikitika mtoto huyo alidai kuwa bibi yake ni mmoja kati ya wanaolima
kando ya ziwa hili kwa muda wa zaidi ya miaka 50 na kuwa alishangazwa kikundi
hicho kuharibu mazao yao ambayo yalistawi vizuri bila hata kupewa taarifa ya
kuwepo kwa utaratibu huo wa kukataza huku wakiwatoza faini ya 50,000 kila
mkulima kitu ambacho ni kinyume na taratibu.
Alisema Bibi
yake alikuwa amekusanya fedha Tsh,30,000 akiwa na lengo la kulipa mahitaji ya
shule lakini watu hao walizichukuwa wakidai kuwa ni faini kitu ambacho
kilipelekea yeye kushindwa kujiunga na masomo hadi pale waandishi wa habari
walipokuja na kuibua utata huo ikiwa ni pamoja na kumuombea misaada kwa watu
mbalimbali ambao waliweza kumsaidia na kumuwezesha kwenda shule.
Mwenyekiti
wa halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kyela mjini kwa upande wake
alisikitishwa na kitendo kilichofanywa na kikundi hicho cha kuwafanyia ukatili
wanakijiji hao kwa kuatoza faini na kuharibu mazao yao kwa madai kuwa walitumwa
na halmashauri kitu ambacho si kweli.
Aliesema kuwa
yeye kama mwenyekiti hanataarifa na uwepo wa mpango huo uliopelekea baadhi ya
watu kuyahama makazi yao kwa kukosa pesa za kulipa faini huku familia zao zikipata
taabu na kwamba suala hilo atalifanyia kazi na kuwashughulikia wale wote
walioendesha opereshen hiyo.
Katika hatua
nyingine Shirika hili linatarajia kufunga mitambo miwili ya kuzalisha Gesi
asilia(BIO GAS) mwisho wa mwezi huu katika kata ya Ipande Tarafa ya Ntebela na
Kasumulu Tarafa ya Unyakyusa kwa ufadhiri wa wakala wa nishati vijijini (REA)
na Shirika lenyewe mradi ambao utapunguza baadhi ya changamoto kwa wananchi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment