Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

March 14, 2014

MWALIMU ATUPWA JELA MIAKA 2 KWA KOSA LA UBAKAJI


Na Ibrahim Yassin,aliyekuwa Nkasi

MWALIMU wa shule ya msingi Katani wilayani Nkasi mkoani Rukwa Ringtone Rayson (36)amehukumiwa kwenda kutumikia kifungo  cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Tshs,100,000 kwa kosa la kufumaniwa na mke wa mtu Beata sangu (31) na kumjeruhi mme wa mwanamke huyo kwa mapanga na msumeno iliyokuwemo ndani ya nyumba hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nkasi Ramadhani Rugemalila mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Hamimu Gwelo alisema kuwa mtuhumiwa mnamo oktoba 12 mwaka jana  majira ya saa 3 usiku mume wa mwanamke huyo  alipata taarifa kutoka kwa msiri wake kuwa mwalimu huyo aliingia ndani ya nyumba yake na kufanya mapenzi na mkewe wakati yeye alipokuwa amekwenda kulala kwa mke mdogo.

Alisema kuwa mume wa mwanamke huyo Richard Feruzi (33) baada ya kupata taarifa hizo alikwenda kumtafuta mdogo wake  Stanslaus Feruzi na viongozi wa mtaa ule kwa lengo la kwenda kumfumania mwalimu huyo na baada ya wote kufika katika nyumba ile walipiga hodi lakini hawakufungua na ndipo walipoanza kuvunja mlango ili waweze kumkamata mtuhumiwa aliyekuwa katika nyumba hiyo.

Mwendesha mashitaka huyo wa jeshi la polisi aliifafanulia mahakama hiyo kuwa wakati mlango ule ulipokuwa ukivunjwa mtuhumiwa ambaye ni mwalimu aliamua kuchukua panga na msumeno vilivyokuwamo katika nyumba hiyo na kuamua kutoka na kuanza kuwashambulia kwa mapanga mume wa mwanamke huyo Richard Feruzi na mdogo wake Stanslaus Feruzi na kuwapatia majeraha makali na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Baada ya mtuhumiwa kukiri kutenda kosa hilo mahakama hiyo ilimuadhibu mtuhumiwa kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Tshs,100,000 na fidia ya Tshs,150,000 kwa kila majeruhi kati ya wale wawili mume na mdogo wa mume kutokana na majeraha waliyoyapata sehemu kadhaa za mwiili yao.

Hakimu wa mahakama hiyo Rugemalila alisema kuwa mtuhumiwa alitiwa hatiani chini ya kifungu  No,225 sura ya 16 ya kanuni ya adhabu hivyo mahakama haikiwa na shaka katika kutoa hukumu hiyo.

Mtuhumiwa baada ya kutiwa hatiani na mahakama hiyo alilipa faini ya Tshs,100,000 na fidia zote na jumla ya Tshs,400,000 zilitolewa katika mahakama hiyo na kuachiwa huru.

Nje ya mahakama baadhi ya wananchi na watu wa karibu na mtuhumiwa huyo walidai kuwa amekuwa na tabia ya kukitembea na wake za watu mara kadhaa na kuwa kutokana na hadhabu ya mahakama na haibu aliyoipata itakuwa somo tosha kwake na kwa wale wenye tabia ya kupenda wake za watu kama yake.
mwisho
Habari hii ni kwa udhamini wa Lukotiko bucher 

 Ni wauzaji wa nyama ya Ng'ombe wa kienyeji wanapatikana wilayani Ludewa.
ufikapo wilayani Ludewa wanapatikana sokoni katika jengo la soko la Samaki.

kwa nyama bora kwaajili ya harusi,sherehe na misiba onana na Lukotiko bucher.
 
Pia wananunua ng'ombe wa kienyeji pahala popote wilayani Ludewa.


kwa nyama bora kwaajili ya harusi,sherehe na misiba onana na Lukotiko bucher.



kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0765878297/0764096248/0765796655 na 0755194056.
kutana na Lukotiko Bucher kwa nyama bora.


No comments: