Deo Filikunjombe akionesha ushirikiano kwa kushikana mikono na Kangi Lugola baada ya kuchangia ununuzi wa gari la parokia ya kanisa Katoliki Ludewa mjini
Mh.Kangi Lugola akiongea na waumini wa kanisa hilo
waumini wa Kanisa katoliki ludewa mjiniwakimsikiliza mbunge wao Deo Filikunjombe
katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Ludewa Bw.Felix Haule akiongea na waumini wa kanisa hilo
Katibu wa mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Stanley Gowele akiongea na waumini wa kanisa hilo
Hizi ni baadhi ya fedha zilizochangwa na Deo filikunjombe katika halambee ya ununuzi wa gari.
MBUNGE wa jimbo la Ludewa katika Mkoa wa Njombe Deo Filikunjombe amefanikiwa kuchangisha papohapo jumla ya shilingi m.30.7 kati ya shilingi m.90 zinazotakiwa na kusakwa na waumini wa kanisa katoliki kwa ajili ya ununuzi wa gari la parokia ya Ludewa mjini.
Harambee hiyo ilifanyika machi mwaka huu katika kanisa la
yesu kristu mkombozi lililopo Ludewa mjini ambapo ilifanyika misa maalumu kwa
kuwashirikisha waumini kutoka vigango vyote vinyounda parokia hiyo ambavyo ni
pamoja na Nyamapinda, Ludewa(K) na Ngalawale.
Ujio wa mbunge huyo ulikuja kufuatia mwaliko wa kamati ya
ununuzi wa gari ambayo ilimtuma diwani wa kata ya Ludewa Monica Mchiro na
mwenyekiti wa kamati hiyo mzee Kayombo kumwomba Filikunjombe kuja kuendesha
harambee hiyo.
No comments:
Post a Comment