baadhi ya madarasa yaliyoezuliwa na mvua
wanafunzi wakiwa darasani chini ya mwembe
wanafunzi wakiwa darasani chini ya mwembe
Gari zilizobeba mifuko 50 ya saruji aliyoitoa Deo Filikunjombe ikiwa tayari kwa kupakuliwa shulani hapo
Wanafunzi wakiishusha saruji iliyotolewa na Deo Filikunjombe
Mvua kubwa
iliyoambatana upepo imesababisha maafa makubwa katika shule ya msingi Ludewa
mjini ambapo paa za vyumba vitatu vya madarasa ziliezuliwa vikiwa na wanafunzi
ndani na kusababisha wanafunzi hao kusomea chini ya mwembe shuleni hapo.
Akitoa
taarifa ya maafa hayo mwalimu mkuu wa shule hiyo John Mjujulu alisema shule
hiyo ni kongwe kwa wilaya ya Ludewa kwani ilijengwa mwaka 1945 tokea hapo
haikuweza kufanyiwa ukarabati wa kuzibadirisha rati chakavu na kuziweka
nyingine hali iliyosababisha shule hiyo kuezuka kwa urahisi.
Mwalimu
Mjujulu alisema maafa hayo yalikuja wakati wanafunzi wakiendelea na masomo
lakini hakuna mtoto aliyejeruhiwa zaidi ya uharibifu wa magunia 24 yenye madebe
tisa ya mahindi yalinyeshewa na mvua ambayo yatengwa kwaajili ya chakula cha
wanafunzi.
Uharibifu
mwingine alioutaja ni pamoja na kuezuliwa kwa paa,bati na lati katika vyumba 3
vya madarasa bati hizo ni chakavu hazifai kuezekea tena,kuta za vyumba vitatu
zina nyufa ambazo zinahitaji ukarabati hali ambayo inahitaji michango ya hali
na mali ili kuwanusuru wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili ambao wanasomea
chini ya mwembe kwa sasa.
“Tunamshukuru
Mwenyezi Mungu kuta za madarasa hayo hazikuwaangukia wanafunzi,kama unavyowaona
wanafunzi wanasomea chini ya mwembe kwa kua leo kunajua lakini ikifika mvua ni
shida tena lakini wameshakuja wataalam kufanya tathmini ukarabati unahitaji
kiasi cha shilingi milioni 12.5 na shule yetu haina uwezo huo hivyo tuawaomba
wadau mbalimbali waliosoma katika shule hii na wengine wenye uwezo wa kutuchangia
watusaidie”,alisema mwalimu Mjujulu.
Aliwataja
walioshiriki katika tathmini ya ukarabati wa shule hiyo kongwe kuwa ni Bright
Komba kutoka idara ya ujenzi katika Halmashauri ya wilaya ya Ludewa na Joseph
Mvanga afisa elimu ufundi ambao kwa umakini mkubwa waliweza kuandika taarifa ya
ukarabati na kufikia kiasi cha shilingi 12.5 milioni.
Aidha
Mwalimu Mjujulu aliweza kutoa shukrani kwa mbunge wajimbo la Ludewa Mh.Deo
filikunjombe kwa kichangia kiasi cha shilingi laki moja na mifuko 50 ya Saruji
ili kuharakisha ukarabati wa madarasa hayo na kuwanusuru wanafunzi wasiweze
kuendelea kusomea chini ya mwembe.
Alisema kama
wadau mbalimbali wataweza kutoa ushirikiano kama alivyoutoa Mh.Filikunjombe kwa
wakati basi anaamini ukarabati huo uatafanyika mapema kwani mpaka sasa bado ni
msimu wa mvua.
Mwalimu
Mjujulu alisema licha ya ukarabati huo wa vyumba vya madarasa matatu pia chule
hiyo inatakiwa kubomoleawa yote mpaka usawa wa madirisha na kujengwa upya
kutokana na shule hiyo kujengwa mwaka 1945 mpaka sasa kwani kuta zake zina
nyufa mabazo ni hatari kwa wanafunzi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment