mama mwasanga akibeba box la malumalu
vifaa vikiombewa ndani ya kanisa
Diwani wa kata ya Ludewa Bi Monica Mchilo akiwajibika
hili ndilo kanisa litakalo fanyiwa ukarabati
Mbunge wa
jimbo la Ludewa Mh.Deo FIlikunjombe ameendelea kutekeleza ahadi zake kwa
wananchi wa jimbo lake pamoja na lengo alilojiwekea la kuvitembelea vijiji
vyote 77 vya wilaya ya Ludewa ili kuweza kuona changamoto vinazowakabili
wananchi.
Akitekeleza
ahadi hizo katika kanisa la Anglikana Ludewa mjini kwa niaba ya Filikunjombe
jana katibu wa mbunge huyo Bw.Stanley Gowele alisema lengo la Filikunjombe ni
kuona ahadi zake alizozitoa kwa wananchi wakati akiomba kura anazitekeleza.
Bw.Gowele
alisema licha ya kuwa Filikunjombe anauguliwa na babayake mzazi kwa kipindi
kirefu akiwa nchini India lakini bado anatafuta fedha za kuweza kutekeleza
ahadi zake kwani kwa kutofanya hivyo atakuwa kawasaliti wananchi wake
waliomchagua kuwa mwakilishi wao.
Akikabidhi
ahadi hizo Gowele aliweza kuukabidhi uongozi wa kanisa la Anglikana mbele ya
waumini wa kanisa hilo jumla ya mifuko 20 ya saruji na katoni 50 za malumalu
vyote vikigharimu kiasi cha shilingi milioni 2.5 ili kulifanyia ukarabati wa
kanisa hilo sehemu ya Madhabahu.
“nimetumwa
na Mbunge wenu Deo Filikunjombe kuwakabidhi vitu hivi vikiwa ni saruji mifuko
20 na malumalu katoni 50 ambazo aliwaahidi kuwaletea,ila amesisitia anaomba
maombi yenu muendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Baba yake mzazi mzee
Filikunjombe ambaye anaumwa na yuko kwa matibabu nchini India”,alisema Gowele.
Aidha katibu
wa kanisa hilo Bw.Stephan Kalinjila Mtweve akishukuru kwa niaba ya waumini wa
kanisa hilo aliweza kumpa pole mbunge huyo kwa kuuguliwa na mzazi wake na
kukili kuwa Filikunjombe amekuwa msikivu
kila uongozi wa kanisa hilo unapojaribu kumshirikisha mambo yao ya kiutendaji.
Bw Kalinjila
alisema kuwa waumini wa kanisa hilo wako bega kwa bega na mbunge wao katika
kila hali kwani wanafanya maombi ili baba mzazi wa mbunge huyo aweze kupona na
kuendelea na majukumu yake ya kila siku kutokana na mzee huyo kuwa na hekma na
busara pale wanapoomba ushauri kutoka kwake.
Alisema
wamekuwa wakimsikia Mbunge wao akitekeleza ahadi zake maeneo mbalimbali katika
jimbo lake na hatimaye nao pia wameweza kutekelezewa kama alivyo waahidi hali
hiyo inawatia moyo wananchi wa wilaya ya Ludewa na kuamini mwakilishi wao
anawajali katika matatizo waliyonayo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment