Misitu ya asili iliyoko kijiji cha Njelela
Wajumbe wa shirika la LCBA wakiandaa mazingira ya upimaji wa maji ya mto Lupali
misitu ya mto Lupali
Mtaalamu wa upimaji Bw.Msumani akiendelea na upimaji wa maeneo ya mto Lupali
Shirika la Ludewa Capacity Bulding
Association (LCBA) lenye makao yake makuu wilayani Ludewa mkoani Njombe kupitia
wakala wa umeme vijijini(REA) linatarajia kufanya upembuzi yakinifu katika
vijiji 19 ili kusambaza nishati ya umeme.
Akiongea na waandishi wa habari
katibu wa shirika hilo Bw.Joseph Kayombo alisema shirika lake linatarajia
kuuzalisha umeme huo kupitia maporomoko ya Mto Lupali ulioko katika kijiji cha
Njelela kata ya Mundindi wilayani Ludewa na kusambaza vijiji 19.
Bw.Kayombo alisema kazi hiyo ya
upembuzi yakinifu itafanyika kwa muda wa miezi sita ambapo tayari wataalamu
kutoaka REA wameshavitembelea vijiji hivyo na kujiridhisha kutokana na andiko
la kuomba fedha za kazi hiyo lililoandikwa na shirika lake.
Akivitaja vijiji vitakavyofanyiwa
upembuzi yakinifu na kunufaika na huduma hiyo ya umeme Bw.Kayombo alisema
katika kata ya Mundindi kijiji cha Mundindi,Amani na Njelela,kata ya Ibumi ni
kjiji cha Ibumi na Nyamalamba kata ya Madilu ni kijiji cha
Madilu,Ilininda,Ilawa,Mfalasi na Manga kata ya Madope kijiji cha
Madope,Luvuyo,Lusitu na Mangalanyene.
Vijiji vingine ni
Mkongobaki,Lipangala,Ugela,Shaurimoyo na Mdilidili hata hivyo alisema umeme huo
utakuwa na nguvu kubwa hivyo unaweza kusambaa katika vijiji vingi zaidi
itakavyowezekana kutokana na wafadhiri wa mradi huo watakavyopendekeza.
“Tumeshafuata hatua zote za kisheria na REA wanatutambua
hivyo wananchi wanapaswa kujenga nyumba nzuri za kudumu ili wajiandae na ujio
wa neema hivyo ya umeme hivyo kwa awali tunatarajia kufanya upembuzi yakinifu
usiozidi miezi 6 ndipo ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme na njia za umeme
itafuata”,alisema Bw.Kayombo.
Diwani wa kata ya Mundindi kupitia
chama cha Mapinduzi ambako umeme huo utazalishwa Bw.Vicent Mgina aliwataka
wananchi wa vijiji hivyo kuwaunga mkono wataalamu watakao fanya kazi hiyo ya
upembuzi yakinifi ili kuharakisha mchakato huo.
Mh.Mgina alisema wananchi wake
kupitia umeme watapata fulsa ya kufanya biashara mbalimbali na kuanzisha
viwanda vidogo vidogo ili kujipatia kipato kwa umeme huo utaenda sambamba na
ujenzi wa chuo cha VETA katika kijiji cha Shaurimoyo hivyo watakaosoma chuo
hicho wataweza kujiajiri kwa kuanzisha karakana zao.
Aidha mjumbe wa shirika la LCBA
Bw.Lazaro Mwinuka alifafanua kuwa shirika hilo unakadiliwakutumia kiasi
cha shilingi 92 Bilion kutoka Bank ya Dunia kupitia REA ambazo zitafanya kazi
zote mpaka mradi huo utakapo kamilika.
Bw.Mwinuka alisema mchakato wa mradi
huo umeshaanza lakini unatarajia kumamilika ifikapo mwaka 2014 kutokana na
ukubwa wa mradi hivyo wananchi wa vijiji tajwa wanatakiwa kuanza maandalizi
katika nyumba zao ili waweze kunufaika na mradi huo.
Alisema mpaka sasa ni kiasi cha
shilingi 350 milioni ndicho kitakachotumika katika kazi za upembuzi yakinifu
katika vijiji hivyo 19 ambapo fedha hizo ni kutoka kwa wakala wa umeme vijijini
(REA)
Hata hivyo Bw.Donota Mgeni maarufu
kwa jina la Ndicheliwe mfanyabiashara wilayani Ludewa na mjumbe wa LCBA alisema
wananchi wenye shughuri zao eneo la mradi watalipwa fidia zao mapema mwaka huu
ili kupisha mradi huo.
Bw.Mgeni alisema kinachotakiwa kwa
wananchi ni kutoa ushirikiano kwa viongozi wa vijiji na kata husika
wanashirikishwa kwa kila jambo ili waweze kutambua manufaa ya umeme huo katika
vijiji na kata zao na si vinginevyo.
Aliwataka kutokuwa na wasiwasi na
shirka lao kutokana na wananchi hao kudanganywa na mashirka mengi yaliyowahi
fika katika mapolomoko hayo na kuahidi yataweka umeme lakini hayakutimiza ahadi
hizo na kutokomea kusikojulikana.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment