Waziri wa Elimu mh.Shukuru Kawambwa akihutubia wananchi mkoani Njombe
Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe akiwa na kitabu cha Njombe baada ya kukabidhiwa na Rais Kikwete
Mama Salma Kikwete akiwasalimia wananchi wa Njombe katika uzinduzi wa mkoa huo
Rais akipata maelekezo jinsi kiwanda cha Chai Lupembe kilivyoanzishwa
Wanafunzi wakiwa katika haraiki siku ya uzinduzi wa mkoa wa Njombe
Rais Kikwete akiwa na profesa Mwaliosi ambaye alikiandaa kitabu cha Njombe
Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amewahakikishia
wananchi mkoani Njombe ujenzi wa Soko la kimataifa katika mji wa Makambako
ambao utaanza hivi karibuni ili kuweza kuwasaidia wananchi wa nyanda za juu
kusini kufanya biashara za mazao yao katika hatua ya kimataifa.
Akikabidhi
hati za ujenzi wa soko hilo kwa viongozi wa mji wa Makambako katika sherehe za
uzinduzi wa mkoa wa Njombe jana Rais Kikwete alisema soko hilo ni la pili
kujengwa nchini wakati jingine lilishajengwa mkoani Arusha ambalo limeonesha
mafanikio makubwa kwa wafanyabiashara nchini.
Alisema
mzinduzi wa mkoa wa Njombe uendane na kasi ya ukuaji wa maendeleo kwa wananchi
ikiwemo ujenzi wa viwanda ambavyo vitawawezesha wananchi kusindika mazao yao na
kuongeza bidii katika uzalishaji ambao utaenda sambamba katika bishara ya
kimataifa ndani ya soko hilo.
Akizungumza
katika sherehe za uzinduzi wa mkoa huo zilizofanyika jana katika viwanja vya
sabasaba mkoani humo Rais Kikwete aliitaja mikoa ambayo inauwezo wa kuzalisha
mazao mbalimbali ikiwemo ufugaji wa ng’ombe wa maziwani pamoja na mikoa ya
Njombe,Mbeya,Rukwa,Iringa na Ruvuma ambayo itanufaika na soko hilo.
Alisema
ifike wakati maziwa yasiagizwe nchi nyingine bali nchi jirani zinapaswa
kuyanunua maziwa hayo nchini kwani kunauwezekano mkubwa katika maeneo ya Kituro
wilayani Makete pakatumika kama sehemu mojawapo ya uzalishaji wa ng’ombe na kuwauzia
wananchikwa bei rahisi ili waweze kufanya biashara ya maziwa kimataifa.
“Serikali
itafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha wananchi wa mkoa huu na mikoa
yenye hali ya hewa nzuri kama hii ya Njombe
wameze kuwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa na kulima mazao yenye tija
ambayo yatawawezesha kulitumia soko lao kwa ufanisi zaidi ili kujikwamua na
ugumu wa maisha uliokithiri miongoni mwa wananchi”,alisema Rais.Kikwete.
Awali kabla
ya kuzindua mkoa Rais Kikwete aliweza kufanya ziara ya kutembelea kata ya
Lupembe mkoani humo ambapoaliweza k uzinduzia kiwanda cha kusindika majani ya
chai kutokana na kata hiyo kutokua na kiwanda cha usindikaji wa majani hayo ya
chai hali ambayo ilikuwa ikiwatesa wananchi wa eneo bilo.
Kiwanda
hicho ambacho kimejengwa na mwekezaji kutoka nchini India kimekuwa mkombozi
kutokana na wananchi wa maeneo ya kata ya Lupembe kutegemea zao hilo katika
uchumi wao hali iliyokuwa ikiwalazimu kusafirisha chai hiyo hadi Njombe ili
kupeleka kiwandani.
Kuhusiana na
miradi ya maendeleo Rais Kikwete aliwasifu wananchi wa mkoa wa Njombe kwa
kushirki kikamilifu katika kuleta maendeleo mkoani hapo kwani aliweza kujionea
wananchi wanavyoweza kujishughurisha katika kujinasua katika wimbi la umaskini
kwakufanyakazi zenye ufanisi kwa mwananchi mmoja mmoja.
Alisema
Serikali imeona juhudi binafsi kwa wananchi hivyo watarajie kuungwa mkono na
Serikali yao katika kila hatua ya maendeleo ikiwemo upande wa Afya,Elimu na
Miundombinu kwani kwani upande wa mindombinu tayari barabara ya Njombe Lupembe
imeshafanyiwa upembuzi yakinifu kwa ajiri ya ujenzi wa kiwango cha lami.
Alizitaja
barabara nyingine ambazo zitajengwa kwa kiwango cha Lami katika mkoa wa Njombe
ili kurahisiha bidhaa kuweza kufika haraka katika soko la kimataifa
linalojengwa Makambako ni pamoja na barabara ya wilaya ya Makete ambayo itaweza
kusafirisha mbao na mazao mengine .
Kuhusu
barabara ya wilaya ya Ludewa alisema hilo halikwepeki kutokana na wilaya hiyo kuwa na migodi mikubwa ya
machimbo ya Makaa ya mawe Mchuchuma na
ujenzi wa kiwanda cha chuma Liganga inayatarajia kutekelezwa hivi
karibuni na wawekezaji wa M.M.I na kampuni wan chi ya China.
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete yuko mkoani Njombe katika ziara ya siku sita ambapo aliwasili
mkoani humo Oktoba 17 mwaka huu ambapo ameweza kufanya kazi ya uzinduzi wa mkoa
huo na baadhi ya miradi ya maendeleo na anatarajia kuzitembelea wilaya zote za
mkoa huo na kuhitimisha ziara yake Oktoba 22 mwaka huu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment