Mkazi wa kitongoji cha Lamya Kijiji
cha Mpunguti Kata ya Katumbasongwe Wilayani Kyela Mbeya Godfrey Mwamwenda (20)
amefariki dunia kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa
kuiba Ng:ombe katika Kijiji cha Lupembe Kata ya Ikolo Wilayani hapa.
Akizungumza na Tanzania Daima leo
(jana) Afisa mtendaji wa Kijiji cha mpunguti Kata ya Katumbasongwe Lusajo
Mwakapiso alisema tukio hilo lilitokea saa mbili usiku wa kuamkia leo baada ya
mashuhuda kumuona akisafirisha ng”ombe huyo nyakati za usiku na ndipo
walipomtilia shaka na kuanza kumdadisi.
Alisema walifikia hatua hiyo ya
kumuuliza kuhusu uhalali wa Ng:ombe huyo baada ya kusikia kuwa kuna Ng”ombe kaibiwa
na ndipo walipopiga mayowe ya kuashiria mwizi na kuwa baada ya mayowe hayo
wananchi walifika kwa wingi na kuanza kushambulia kwa fimbo na mawe hali
iliyopeleke kufariki dunia papo hapo.
Aliongeza kuwa baada ya kutokea
tukio hilo walilijurisha jeshi la Polisi ambao walifika katika eneo hilo na
kuuchukua mwili huo na kuupeleka katika hospitali ya Wilaya ya Kyela kwa
uchunguzi zaidi.
Ndugu wa karibu na marehemu
huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa Kijana huyo ambaye alikuwa
akisoma shule ya sekondari ya Ikolo aliacha shule akiwa kidato cha pili na kuwa
alianza vitendo hivyo katika familia yake ambapo katika siku za nyuma aliwahi
kuiba Ng:ombe wa baba yake aliyemzaa.
Katika hatua nyingine Mkazi wa
kitongoji cha Mwakikome kijiji cha Mpunguti kata ya Katumba songwe Wilayani
hapa Julius Mwambelo (38) amefarika dunia baada ya kugongwa na gari katika
barabara itokayo Kyela kwenda Katumba songwe.
Kwa mujibu wa afisa Mtendaji wa
Kijiji hicho Lusajo Mwakapiso ni kuwa tukio hilo limetokea leo saa 5 hasubuhi
wakati mtu huyo akivuka barabara na ndipo gari hilo aina ya Center lenye namba
za usajili T.318 BHY lililokuwa limebeba mtumbwi likitokea kyela mjini kuelekea
Katumba songwe likipeleka mtumbwi katika ziwa nyasa.
Mashuhuda waliokuwepo katika eneo
hilo la ajali hiyo walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva
na kuwa alionekana kushindwa kulimudu gari hilo kutokana na vumbi iliyotanda
katika barabara hiyo.
Mganga wa zamu aliyekuwepo katika
hospitali ya Wilaya ya kyela Dk.Nsubili Mwansule mbali na kukiri kupokea miili
hiyo pia alisema kuwa mtu huyo aliyegongwa na gari alifariki dunia baada ya
kuumia huku damu ikivuja ndani kwa ndani,na aliyepigwa kwa wizi alikua
ameumizwa vibaya katika sehemu kadhaa katika mwili wakekutokana na kipigo hali
iliyopelekea kifo chake.
Jeshi la polisi Wilayani Kyela
limedhibitisha kuwepo kwa matukio hayo na kuziruhusu failia hizo kuendelea na
taratibu za mazishi huku wao wakiendelea na uchunguzi.
Mwisho.
Na Ibrahim Yassin,Kyela
No comments:
Post a Comment