Baadhi ya mahindi ambayo yameshanunuliwa
Wakulima wilayani Ludewa katika mkoa wa
Njombe wameanza kutoa malalamiko kutokana na kutolipwa fedha zao kwa
wakati kutoka kwa wakala wa hifadhi ya chakula Taifa(Nation Food
Reseve Agents)kwani mategemeo yao ni kuuza mahindi na kupata fedha
kwa wakati ili waweze kuwalipia watoto wao michango ya shule.
Akitoa malalamiko hayo mmoja mmoja wa
wakulima wilayani hapa Bw.Mathayo Mwinuka alisema kuwa kumekuwa na
ucheleweshaji mkubwa wa malipo tofauti na awali ambapo ilikuwa
haidizi muda wa wiki moja baada ya kupima mahindi na kupewa fundi
wakulima kulipwa fedha zao.
Bw.Mwinuka alilalamikia hilo kutokana
na mamlaka hiyo inayonunua mahindi wilayani Ludewa na wilaya nyingine
nchini kukaa na fedha za wakulima wa mahindi wilayani humo zaidi ya
wiki tatu hivi sasa bila ya kuwalipa wakulima hao ambao hutegemea
fedha hiyo katika kulipia ada watoto wao na matumizi ya kila siku.
“Inashangaza kuona tunauza mahindi
ili tuweze kutatua matatizo yetu haraka lakini tunacheleweshewa
malipo yetu mpaka watoto wetu wanafukuzwa mashuleni na kuzuiliwa
kufanya mitihani kutokana na kukosa ada,kwani awali tulikuwa tukiuza
mahindi na kupata fedha kwa wakati hivyo tunaomba Serikali
kuliangalia hilo sisi si wakulima wa kahawa ambao huchukua fedha kwa
msimu”,alisema Bw.Mwinuka.
Alisema mpaka sasa ni wananchi wengi
ambao wameuza mahindi yao katika mamlaka hiyo hawajapata fedha lakini
wako wengine waliowauzia walanguzi tayari wameshalipwa fedha zao kwa
wakati hali inayowakatisha tamaa wakulima wengine kupeleka mahindi
katika mamlaka hiyo wakihofia kucheleweshewa fedha zao.
Aidha Msimamizi wa manunuzi wa mamlaka
ya NFRA katika kituo cha Ludewa mjini Bi.Rose Mbuya aliwataka
wakulima hao wasiwe nawasiwasi kuhusiana na malipo ya mazao yao kwani
kulikuwa na matatizo kidogo katika ofisi ya kanda Makambako lakini
tatizo hilo limesha tatulika na hivi punde malipo hayo yatafanyika.
Bi.Mbuya alisema mpaka sasa mahindi
yaliyonunuliwa ni zaidi ya tani 64501 na bado mahindi yanaendelea
kununuliwa hivyo wakulima wanashauliwa kuendelea kupeleka mahindi yao
ili yapimwe mapema bila kujali fedha za awali bado hazijalipwa kama
wanavyolalamika.
Alisema kuwa wamepokea malalamiko mengi
yakiwemo ya kutotenda haki katika upimaji na wengine kukataa kukatwa
kiasi kilo moja na nusu kwaajili ya uchafu wa mahindi
wanayoyaleta,hizo zote ni changamoto tu lakini malipo yao yatafanyika
hivi karibuni.
“ni kweli wakulima hawajalipwa kwa
muda mrefu na tunakili tumewaharibia malengo yao lakini wasihofu
walipo yatafanyika ila kitu cha msingi ni kwamba wasikatishwe tamaa
na hali hii iliyotokea sasa,kulikuwa na matatizo kidogo katika kituo
cha Makambako ila hali imeshatengamaa nawashauri waendelee kuleta
mahindi yao malipo yatafanyika”,alisema Bi.Mbuya.
Bi.Mbuya alisema wanakumbana na
changamoto nyingi katika manunuzi ya mahindi ikiwemo ya wakulima
kuleta mahindi machafu yenye fumbi na kugomea wanapopewa utaratibu wa
kufanya kutokana na hali hiyo imekuwa vigumu kuwaelimisha wakulima
hao kutokana na wao kuona hawatendewi haki.
Mwisho.
habari hii ni kwa udhamini wa Lukotiko bucher.Ni wauzaji wa nyama ya Ng'ombe wa kienyeji wanapatikana wilayani Ludewa.
ufikapo wilayani Ludewa wanapatikana sokoni katika jengo la soko la Samaki.
kwa nyama bora kwaajili ya harusi,sherehe na matatizo mbalimbali onana na Lukotiko bucher.
Pia wananunua ng'ombe wa kienyeji pahala popote wilayani Ludewa.
kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0765878297/0764096248/0765796655 na 0755194056.
kutana na Lukotiko Bucher kwa nyama bora.
No comments:
Post a Comment