MAHAKAMA
ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe imemhukumu kwenda jela
miaka thelathini na kuchapwa viboko 30 matakoni mwalimu Romanus
Msango wa shule ya msingi Ingwachanya na mkazi wa Lupembe wilayani
Njombe kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa miaka 14 na kumuumiza vibaya
katika sehemu za mwili wake.
Akisoma
hukumu hakimu mkazi mfawidhi katika mahakama ya wilaya ya Ludewa
Fredrick Lukuna alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na
upande wa mashtaka na kwamba hakuna shaka lolote katika kuthitisha
mshtakiwa kutenda kosa hilo linaloangukia katika kifungu namba
1309(1) na 31(1) kaanuni ya adhabu zuzu ya mwaka 2002.
“””” pamoja
na kuwa mshtakiwa ni mkosaji wa kwanza na kwa kuzingatia taaluma ya
mshtakiwa na makosa haya kushamili katika jamii ya wana Ludewa,
matendo haya yakiachwa yanaweza kuleta athari kwa watoto na wananwake
ikiwemo magonjwa ya kuambukizwa. Natoa amri utakwenda jela miaka 30
na viboko thelethini.””” aliamuru Lukuna
Awali
ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka mratibu wa polisi
Edison Kasekwa(SP) kuwa mshtakiwa Romanus Msango alitenda ukatili huo
wa kinyama Augost 20 mwaka jana katika kijiji cha Masimbwe kata ya
Mlangali ambapo kabla ya kutenda kosa hilo alimshambulia mhanga na
kisha kubaka na kumlawiti na kumsababishia maumivu makali mwilini.
‘’’’’’ hakuna
makosa ya awali kwa mshtakiwa hata hivyo serikali ilimpa dhamana
kubwa ya kulea watoto ambao ni nguvukazi ya Taifa la kesho lakini
amewageuka na kutenda kitendo kinyume na maadili ya kazi yake na
kuidharirisha taaluma pamoja na serikali naomba mahakama itoe adhabu
kali ili liwe fundisho kwa walimu wenye tabia kama hii’’’’’
alihitimisha Kasekwa
Kasekwa
aliongeza kuwa mshtakiwa alikusudia kutenda makosa hayo kwa sababu
alimfuata mwanafunzi huyo shambani alikokuwa akivuna mahindi na
wenzake ambao walikimbia kwenda kijiji kutoa taarifa baada ya mwalimu
kumkamata mwenzao na kumpeleka kichakani.
Wakati
huohuo watu wawili Bahati Mtega na Flowin Mtweve wakazi wa Milo
wamehukumiwa kifungo cha maisha na kuchapwa viboko 12 kila mmoja kwa
kosa la kumbaka kwa pamoja mtungo au (gang rape) Ester Mchiro makosa
yanayoangukia katika kifungu cha 131(A).
Watuhumiwa
hao walimbaka Bi. Ester Mchiro ambaye ni mke wa mtu hali ambayo
ilisababisha mama huyo kupiga kelele na kuomba msaada ndipo raia wema
walipokusanyika na kumkamata moja wa wabakaji hao na kumshikisha
adabu kabla ya kumpeleka kituo cha Polisi Lugarawa ambapo mtuhumiwa
mmoja alitimua mbio.
No comments:
Post a Comment