Mchekeshaji mahili Bw.Kinyambe naye pia atakuwepo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa
Mchekeshaji Kinyambe akiwa katika moja ya kazi zake
Warembo
wilayani Ludewa wanatarajia kuchuana vikali ili kumsaka miss
Ludewa 2013 kutokana na wilaya hiyo kutofanya tamasha kama hilo tokea
Tanzania ilivyopata uhuru hivyo itakuwa Historia kwa warembo hao
kuibuka na ushindi utakaoambatana na zawadi nono na kuendelea
kuiwakilisha wilaya katika ngazi nyingine.
Tamasha hilo la kumsaka mrembo au miss Ludewa litakalofanyika wilayani humo hivi karibuni limeandaliwa na MAHELEN na SISTER T.kwa lengo la kumtafuta mrembo atayeiwakilisha wilaya ya Ludewa katika ngazi ya Mkoa wa Njombe na baadae Taifa.
Fomu za shindano hilo zimeshaanza kuchukuliwa na
wanyange hao lakini bado nafasi za ushiriki wa tamasha hilo zipo
hivyo kwa yeyote anayehitaji kushiriki fomu zinapatikana maeneo
yafuatayo:
1.Ludewa-Maheleni studio stend kuu ya mabasi Ludewa
mjini.
2.Radio
Best FM 90.5 Ludewa mjini
3.Manda-onana na Basil Ngailo
4.Luilo-onana na Mh.Diwan Kongo
5.Mawengi-Kivulini Grocery
6.Lugarawa-Chuo cha Maabara
7.Mlangali-onana na Sija M-PESA
8.Amani-Anazeti Grocery
SHINDANO HILO LITAFANYIKA TAREHE 6/09/2013 KATIKA
UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA.
Wanyange hao kabla ya siku ya shindano watapata fulsa
ya kutembelea migodi ya chuma cha Liganga na Makaa ya Mawe
Ng'omang'ombe na Fukwe za ziwa Nyasa.
KWA WALE WALIOCHUKUA FOMU KAMBI ITAANZA TAREHE
3/9/2013.
TAMASHA HILO LITASINDIKIZWA NA WASAII RUKUKI
WAKIWEMO,MCHEKESHAJI KINYAMBE KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM,SAMILI
KINYULINYULI NA KIKUNDI CHA SARAKASI KUTOKA MBAGALA DAR ES SALAAM PIA
WASANII WA NDANI YA WILAYA YA LUDEWA.
KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISI YA MAHELENI STUDIO STEND
KUU YA BASI LUDEWA MJINI AU PIGA SIMU NO.0767680596/ 0757581177 au
0652608677
UNASHAURIWA KUTOA TAARIFA MAPEMA KUPITIA NAMBA HIZO.
Zawadi nono kwa washindi imeandaliwa na wadhamini wa
tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment