MASHINDANO ya Ligi ya Pambana Saidia Jamii kumtafuta
Bingwa wa Wilaya katika mchezo wa Drafti Wilayani Kyela Mkoani Mbeya
yamefikia tamati jana huku Oboti Mwakasungu akiibuka mshindi wa
mashindano hayo na kujinyakulia Mbuzi jike mwenye uza uzito,
Ligi hiyo iliyoshirikisha wachezaji 42 kutoka katika
timu za Tarafa zote mbili Unyakyusa na Ntebela ambayo ilianza kwa
njia ya makundi na baadaye mtoano na jana ilikuwa ni fainali ya
mwisho na kupatikana washindi wane ambao walikabidhiwa zawadi zao.
Katibu wa Chama cha Drafti Wilayani Kyela Jamesi
Mwambungu aliwataja washindi hao kuwa ni Obote Mwakasungu aliyeshika
nafasi ya Kwanza aliyepata Mbuzi Mwenye Thamani ya Tsh,100.000,wapili
alikuwa ni Willy Mwambete aliyepata Kuku wanne jogoo wenye thamani ya
48,000,wa tatu ni Hamis Chengula aliyejipatia kuku watatu tetea wenye
thamani ya Tsh 30,000,na wane alikuwa ni Ibrahim Mwakanyamale
aliyeambulia kuku wa wili tetea wenye thamani ya Tsh,20.000.
Mwambungu pia alitoa zawadi kwa waendeshaji wawili wa
ligi hiyo ambao ni Peter Senge na Danny Mwakila ambao walipewa
shilingi elfu 4,000, kwa kila mmoja.
Mwenyekiti wa Chama hicho Gasper Mwasimba aliwapongeza
washindi hao kwa kuibuka na ushindi na kuwataka wachezaji wengine
kujitokeza kujiunga na mchezo huo ili waweze kushiriki mashindano
mengine pindi yatakapo anza.
Mshindi wa mashindano hayo Obote Mwakasungu alisema kuwa
hakutegemea kama ataibuka na ushindi kwakuwa ligi hiyo ilichezwa na
wachezaji wenye uzoefu hivyo anajisikia furaha yeye kuibuka na
ushindi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asas ya Pambana Saidia jamii
Taifa ambaye ndiye aliyedhamini wa mashindano hayo Abraham Mwanyamaki
alipongeza jitihada zilizofanya na viongozi hao waliofanikisha mchezo
huo na kwamba ataendelea kutoa mchango wake pale utakapohitajika ili
kusaidia kukuza mchezo huo.
Alisema kuwa Ligi ijayo ataboresha zawadi ili kuwavuta
vijana wengi wajiunge na mchezo huo kwa lengo la kupata fursa
ya kuonesha vipaji vyao katika mchezo huo unaotambulika kimataifa.
Mwisho.
Na Ibrahim Yassin,Kyela
No comments:
Post a Comment