Mkuu
wa wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Bw.Juma Solomon Madaha
amezitaka taasisi za Dini nchini kuhubiri amani kwa waumini kwani kwa
kufanya hivyo kutapunguza migogoro ya kidini inayoweza kujitokeza
kutokana na kutovumiliana.
Bw.Madaha
aliyasema hayo jana wakati akifunga mkutano wa Injili katika kanisa
la Anglikana mtaa wa Ludewa mjini,mkutano huo uliwakutanisha wahubiri
mbalimbali wa kutoka mikoa ya Njombe,Mbeya na Mtwara.
Alisema
kutokana na vurugu za chinichini zinatoendelea nchini ambazo ni
pamoja na kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa Dini na uchoamaji wa
nyumba za ibada unaoendelea ni vema taasisi za kidini zikahubiri
amani ili waumini waweze kumrudia Mungu.
Bw.Madaha
alisema kumekuwa na vurugu za chinichini zinazochochea udini hali
ambayo haina tija ndani ya Taifa la Tanzania hivyo waumini wa Dini
zote wanapaswa kuwapuuza wachochezi na wenye lengo la kuwagawa
watanzania kwani hawana nia nzuri na watanzania wenye tabia ya
utulivu.
“waasisi
wa taifa hili yaani Baba wa taifa Mwalimu Nyerere na Shekh.Karume
walisisitiza amani kwa watanzania hivyo nawaomba wahubiri wote
liombeeni taifa letu liwe na amani na waumini wa Dini zote wawe na
moyo wa kuvumiliana kwani hakuna aliye mkamilifu hapa
duniani”,alisema Bw.Madaha.
Bw.Madaha
aliyema Serikali iko bega kwa bega na kazi nzuri zinazofanywa na Dini
zote katika kulijenga taifa hivyo kila muumini wa Dini yoyote
anatakiwa kuhakikisha amani inaendelea kudumishwa kama ilivyozoeleka
kwa watanzania.
No comments:
Post a Comment