Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

August 15, 2013

TAMASHA LA KUMSAKA MISS LUDEWA LATARAJIA KUFANYIKA SEPT 6. 2013



Warembo wilayani Ludewa 2013 wanatarajia kuchuana vikali ili kumsaka miss Ludewa kutokana na wilaya hiyo kutofanya tamasha kama hilo tokea Tanzania ilivyopata uhuru hivyo itakuwa Historia kwa warembo hao kuibuka na ushindi utakaoambatana na zawadi nono na kuendelea kuiwakilisha wilaya katika ngazi nyingine.

Tamasha hilo la kumsaka mrembo au miss Ludewa litakalofanyika wilayani humo hivi karibuni limeandaliwa na MAHELEN na SISTER T.kwa lengo la kumtafuta mrembo atayeiwakilisha wilaya ya Ludewa katika ngazi ya Mkoa wa Njombe na baadae Taifa.

Fomu za shindano hilo zimeshaanza kuchukuliwa na wanyange hao lakini bado nafasi za ushiriki wa tamasha hilo zipo hivyo kwa yeyote anayehitaji kushiriki fomu zinapatikana maeneo yafuatayo:

1.Ludewa-Maheleni studio stend kuu ya mabasi Ludewa mjini.
2.Radio Best FM 90.5 Ludewa mjini
3.Manda-onana na Basil Ngailo
4.Luilo-onana na Mh.Diwan Kongo
5.Mawengi-Kivulini Grocery
6.Lugarawa-Chuo cha Maabara
7.Mlangali-onana na Sija M-PESA
8.Amani-Anazeti Grocery

SHINDANO HILO LITAFANYIKA TAREHE 6/09/2013 KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA.

Wanyange hao kabla ya siku ya shindano watapata fulsa ya kutembelea migodi ya chuma cha Liganga na Makaa ya Mawe Ng'omang'ombe na Fukwe za ziwa Nyasa.

KWA WALE WALIOCHUKUA FOMU KAMBI ITAANZA TAREHE 3/9/2013.

TAMASHA HILO LITASINDIKIZWA NA WASAII RUKUKI WAKIWEMO,MCHEKESHAJI KINYAMBE KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM,SAMILI KINYULINYULI NA KIKUNDI CHA SARAKASI KUTOKA MBAGALA DAR ES SALAAM PIA WASANII WA NDANI YA WILAYA YA LUDEWA.

KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISI YA MAHELENI STUDIO STEND KUU YA BASI LUDEWA MJINI AU PIGA SIMU NO.0767680596/ 0757581177 au 0652608677

UNASHAURIWA KUTOA TAARIFA MAPEMA KUPITIA NAMBA HIZO.

Zawadi nono kwa washindi imeandaliwa na wadhamini wa tamasha hilo.

No comments: