Wafanyabiashara wa Soko Kuu Wilayani Njombe Wamelalamikia Ubovu wa Miundombinu Sokoni Hapo Pamoja na Ukosefu wa Huduma Muhimu Kama Vile Maji na Umeme Hali Ambayo Wamesema Imechangia Kuzorotesha Biashara Sokoni Hapo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wetu Baadhi ya Wafanyabiashara Sokoni Hapo Wamesema Kuwa Ukosefu wa Umeme Sokoni Hapo Umekuwa Ukikwamisha Shughuli Zao Hasa Nyakati za Usiku Kutokana na Kukosa Ulinzi wa Uhakika.
Wamedai Kuwa Kukosekana Kwa Huduma ya Maji Kumesababisha Kushuka Kwa Ubora wa Bidhaa Zinazouzwa Sokoni Hapo Hasa Samaki Ambao Wamekuwa Wakihitaji Sana Maji Ili
Kuweza Kuwa na Ubora Kwa Kipindi Chote Cha Soko
Kutokana na Hali Hiyo Wafanyabiashara Hao Waliiomba Serikali Kuwaboreshea Soko Hilo Kwa Kuhakikisha Upatikanaji wa Huduma ya Nishati ya Umeme na Maji Ambayo Mara Kadhaa Ilikwisha ahidiwa Kuboreshwa Bila Utekelezaji.
Afisa Biashara Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw.Edward Mdemu alikiri Kuwepo kwa Changamoto Hizo Katika Soko Hilo na Kwamba Awali wafanyabiashara Hao waliomba Kuongezewa Mwanga wa Mabati hali iliyopelekea zoezi hilo Kufanikiwa
Pamoja na Mambo Mengine Bw. Mdemu Aliwataka Wafanyabiashara Hao Kuwa wavumilivu na Kwamba atazifikisha Taarifa hizo kwa Mhandisi ili Ashughulikie Tatizo Hilo.
Na
Gabriel Kilamlya Njombe
No comments:
Post a Comment