ALIYEKUWA
mratibu wa Bima ya Afya katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa Mkoani
Njombe Daktari Adamson Ndapisi amefikishwa katika mahakamani ya
Hakimu mkazi kwa makosa tisa ikiwemo kugushi barua na saini za
watumishi wenzake na kujipatia jumla ya shilingi m.3.3 mali ya
serikali.
Mbele
ya hakimu mkazi mfawidhi katika mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick
Lukuna mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
(TAKUKURU) mkoa wa Njombe Richard Marekani akaiambia mahakama kuwa
mshtakiwa Adamson Ndapisi alitenda makosa hayo aprili 2008 akiwa
mratibu wa bima ya afya wilaya.
Katika
shtaka la kwanza marekani akaiambia mahakama kuwa mshtakiwa aligushi
barua ya kuomba shilingi m.3.3 kwa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa
kwa lengo la kuendesha semina hewa kwa watumishi wa idara ya Afyahuku
akijua ni uongo chini ya kifungu 333, 335,(d) 1 kanuni ya adhabu sura
ya 16.
Makosa
mengine ni matumizi mabaya ya madaraka chini ya kifungu 22 kanuni ya
adhabu ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka
2002 ambapo mshtakiwa anatajwa kughushi risiti yenye thamani ya jumla
ya shilingi milioni 2.1 na kuwasainisha watumishi wa idara ya afya
huku akitambua kuwa ni kosa.
Aidha
mfanyabiashara maarufu wa mgahawa wa NAM CAFE ulioko mjini Ludewa
Maria Haule ambaye katika kesi hiyo ni mshtakiwa wa pili anakabiliwa
na kosa moja la kushiriki kuidanganya serikali kwa kutoa risiti za
vyakula hewa zinazoonesha kuwa mshtakiwa alinunua vitu dukani kwake
kosa linaloangukia katika fungu la namba 30 ya sheria ya kuzuai na
kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Washtakiwa
wote walikana kuhusika na makosa yanayowakabili, na kesi imeahirishwa
hadi agosti 19 mwaka huu kesi itakapokuja kusikilizwa kwa
awali.washtakiwa wote waliachiwa baada ya kutimiza masharti ya
dhamana ambapo kila mmoja alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye
mali isiyohamishika isiyopungua thamani ya shilingi milioni sita.
mwisho
Na
Bazil Makungu Ludewa
No comments:
Post a Comment