Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

August 19, 2013

KIJANA AIELEZA MAHAKAMA ALIVYOFANYIWA UNYAMA NA ASKARI, ALINYWESHA MKOJO NA KULAZIMISHWA KUFANYA MAPENZI NA UKUTA.

MSHTAKIWA wa kwanza katika kesi ya kubaka Flown Mtweve mkazi wa kijiji cha Lipangala kata ya Mkongobaki wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe ameishangaza mahakama alipoeleza unyama na ukatiri aliofanyiwa na askari mgambo na polisi oktoba 26 mwaka jana kabla na baada ya kubambikwa kesi ya kubaka mke wa mtu.

Akizungumza kwa uchungu jana mbele ya hakimu mkazi mfawidhi katika mahakama ya wilaya ya Ludewa mheshimiwa Fredrick Lukuna Bw Flowin alisema siku ya tukio alikuwa nyumbani kwake katika kitongoji cha Ngongano, akiwa njiani kuelekea hospitari kumuona mamake mgonjwa njiani alikutana watu wakiwemo askari mgambo ambao walimpiga kwa mapanga na malungu kabla ya kumkamata.

Aliwataja askari mgambo kuwa ni pamoja na Lusius Mtweve, Joseph Mchiro, Ester Mchiro na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Mhagama alikutana nao mjiani wakamlazimisha kulipa deni la shilingi 50, 000 fedha aliyokuwa akidaiwa na Joseph Mchiro na baada ya kujitetea kuwa hakuwa na fedha hiyo na kwamba alikuwa akienda kumwona mgonjwa hospitalini ndipo alianza kushambuliwa kwa mapanga na virungu mwilini.

’’’’’ majira ya saa nane na nusu za usiku nililazimishwa kunywa maji yaliyokuwa kwenye kopo nilipokunywa kumbe ulikuwa mkojo wa mtu mzima na baada ya muda nilianza kutapika nikiwa katika ofisi za kijiji na ilipotimia majira ya saa nane usiku nilipelekwa katika kituo cha polisi Lugarawa ambako askari aliyekuwa zamu alinivua nguo na kunilazimisha nifanye mapenzi na ukuta mpaka nimalize haja zangu ’’’’’ alilalamika Flowin

Alieleza mahakama kuwa mkuu wa kituo cha polisi Lugarawa ambaye hata hivyo hakulitaja jina lake kwamba alipokuja asubuhi alimkemea askari aliyekuwa zamu usiku ule na kumwonya kwa kumwamru anipe karatasi ya polisi kwa ajili ya matibabu (PF) kwa kuwa nilikuwa nimeumia vibaya na kisha kunipeleka katika hospitari ya misheni ya Lugarawa ambako alilazwa kwa muda wa wiki mbili akitibiwa majeraha yaliyotokana na kupigwa na mapanga kabla ya kubambikwa kesi ya kubaka.

Awali mshtakiwa aliieleza mahakama kuwa ni kweli alikuwa akidaiwa na mtu aitwaye Joseph Mchiro ambaye ni mume wa Ester Mchiro ambaye ndiye anayedaiwa kubakwa na mshtakiwa Flowin Mtweve na kwamba katika tukio hilo alinyang’anywa jumla ya shilingi 48,000 taslimu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi agost 19 mwaka huu itakapokuja kwa kusikilizwa. Kesi iliahirishwa baada ya mwendesha mashtaka mratibu wa polisi SP Kusekwa kuomba muda ili akaipitie kesi hiyo kwa sababu hapo awali kesi hiyo ilikuwa ikiendeshwa na mtu mwingine.

mwisho


No comments: