.
aliyetangulia mbele ni Afisa mtendaji wa kijiji cha Ludende wakihamasisha wananchi katika shughuri ya uchimbaji barabara
WANANCHI wa kijiji cha
Ludende kata ya Ludende wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe
wameamua kuchimba barabara itakayo wasaidia kusafirisha mazao yao
kutoka kijijini hapo na kuyapeleka sokoni ili kukwepa mlima katika
barabara ya awali ambayo walitumia gharama kubwa wakati wa kukodi
vyombo vya moto.
Uchimbaji wa barabara hiyo
umekuja baada ya barabara waliyokuwa wakiitumia kuwa na mlima mkali
hali ambayo ilikuwa ikisababisha gari za mizigo kushindwa kupanda
mlima huo zikiwa na mzigo na kusababisha gharama kubwa ya
usafirishaji wa mazao.
Akizungumza jana
Mwenyekiti wa kijiji cha Ludende Bw.Samwel Shagama alisema ni kwa
muda mrefu kijiji hicho kimekuwa kisiwani kutokana na barabara hiyo
kuwa na mlima mkali hivyo wananchi wameamua kujitolea kwa nguvu zao
ili kuchepusha barabara hiyo.
Bw.Shagama alisema licha
ya gharama za usafirishaji wa mazao pia hata gharama za kukodi
bodaboda kutoka kijijini hapo na kupeleka wagonjwa katika kijiji cha
jirani cha Milo ambako kuna Hospitari kubwa hali ilikuwa vivyo hivyo.
“uanzishwa wa barabar
hii inayounganisha kijiji cha Ludende kwena kata ya Milo hadi
barabara ya Kigasi ni ukombozi mkubwa kwani tumekuwa tukinyanyasika
mno kwa bei kubwa hasa kwa wamiliki wa vyombo nya moto”,alisema
Bw.Shagama.
Alisema kutokana na
manyanyaso hayo wananchi kwa umoja wao na kwa hiari yao waliamua
kufanya utafiti wapi barabara hiyo itapita na kufikia muafaka ambao
umepelekea kuichimba barabara hiyo haraka bila ya kuomba msaada
Serikalini.
Aidha afisa mtendaji wa
kijiji hicho Bw.Timoth Mwinuka alisema barabara hiyo iliyochimbwa na
wananchi ni nyembamba hivyo inahitajika upanuzi kwa kutumia mashine.
Bw.Mwinuka alisema suala
la upanuzi ili kuwaungamkono wananchi wa kijiji cha Ludende
atalifikisha katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya
Ludewa kwani barabara hiyo ni kubwa ambayo inaunganisha zaidi ya kata
nne.
Alikubali kuwa awali
wananchi wakijiji hicho walishindwa kusafirisha mazao yao bamoja na
wagonjwa pindi inapotokea dharula kutokana na barabara ya awali kuwa
na mlima mkali ambao ulikuwa hatari zaidi lakini kwa kuchepucha
katika kuukwepa mlima huo imekuwa nafuu zaidi.
Bw.Mwinuka aliwataka
wananchi wa kijiji cha Ludende na vijiji jirani kuitunza barabara
hiyo kwa kutopitisha mifugo ili siku wakifika wataalamu kutoka
Serikalini kwaajili ya kuikagua waikute ikiwa katika hali nzuri.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment