Afisa utumishi wilaya ya Ludewa Bw.Horace Kolimba akihutubia wananchi
Mwenyekiti mstaafu wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mzee Hilaly Nkwera akiwasalimia wananchi
Burudani ya ngoma ya mganda ya kikundi cha mzalendo ikiendelea kuburudisha
vijana wakijiandaa katika shindano la kunywa soda
Afisa maendeleo ya jamii wa wilaya ya Ludewa Bw.Malima akitoa mkono wa pongezi kwa mshindi wa shin dalo la kukimbiza kuku
Afisa utumishi Horace Kolimba akisoma taarifa ya halmashauri ya wilaya ya Ludewa
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bi.Mwano aliyesimama katikati akijiandaa kupokea maandamano ya wafanyakazi wa Serikali za Mitaa
Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Chalamila aliyetangulia akifuatiwa na Hakimu wa wilaya ya Ludewa Mh.Lukuna
kikundi cha ngoma ya ngwaya kikijiandaa kutumbuiza
HALMASHAURI
ya wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe, katika kipindi cha julai 2012 hadi
juni 30, 2013 imetumia jumla ya shilingi 1.3bilioni katika shilingi
3.3bilioni zilizokisiwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya maendeleo fedha iliyotolewa na serikali pamoja na wahisani
mbalimbali.
Taarifa
hiyo ilitolewa jana katika kilele cha maadhimisho ya siku ya serikali
za mitaa iliyofanyika julai mosi mwaka huu katika uwanja wa mpira wa
miguu Ludewa mjini ambapo pamoja na mambo mengine halmashauri ilitoa
ufafanuzi wa mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013.
Akitoa
taarifa kwa wananchi kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya
ya Ludewa, afisa utumishi na utawala Horace Kolimba alisema kuwa
maadimisho haya yanafanyika katika kila ngazi kuanzia
Taifa,Mkoa,Wilaya, Kata, Kijiji hadi kitongoji na kwa upande wa
Ludewa maadhimisho yameenda sanjari na shughuli za ujenzi wa Taifa
yakiwemo maonesho,burudani na hotuba kutoka kwa viongozi.
No comments:
Post a Comment