Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

July 02, 2013

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AWATAKA WANANCHI KUJITOKETA KATIKA MAPOKEZI YA WAZIRI MKUU



 Mkuu wa mkoa wa Njombe Kepten Mstaafu Asery Msangi akihutubia wananchi

 kushoto mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha akijadiliana jambo na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Wiliam Waziri



 MKUU wa Mkoa wa Njombe Captain mstaafu Asheri Msangi amewataka wananchi wa Ludewa kujitokeza kwa wingi julai 10 mwaka huu katika uwanja wa mpira wa miguu mjini Ludewa kumpokea na kumsikiliza waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Peter Kayanza, anayetarajia kufika wilayani hapa kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kutembelea migodi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga.

Mheshimiwa Msangi aliyasema hayo jana katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Serikali za mitaa yaliyokuwa yakiendelea katika uwanja wa mpira wa miguu mjini Ludewa.

Mkuu wa mkoa alifika katika uwanja huo huku maadhimisho yakiendelea na kulazimika kusimamisha shughuli hizo kwa muda ili kusikiliza maelekezo ya mkuu huyo juu ya ziara muhimu ya waziri mkuu wilayani hapa.

Pamoja na kutoa taarifa ya ziara ya waziri mkuu mheshimiwa msangi aliwataka viongozi kuwaruhusu wananchi kuuliza maswali kama hawataridhika na taarifa itakayotolewa na Halmashauri kama watakuwa hawajaridhika.

Kwa mjibu wa mkuu huyo wa mkoa wa njombe waziri mkuu atawasili wilayani Ludewa julai 10 mwaka huu majira ya asubuhi ambapo ataanza kukagua kinu cha kukoboa kahawa katika kata ya mawengi na kumalizia shule ya sekondari Kidulile kuangalia vyumba vya madarasa kwa ajili ya kidato cha tano na sita.

Waziri Mkuu atalala mjini Ludewa na kesho yake julai 11 atatembelea mgodi wa chuma cha Liganga kilichopo katika kata ta Mundindi na kuelekea njombe. Mkuu wa mkoa alitembelea wilaya ya Ludewa kukagua njia na barabara atakayopita waziri Mkuu.

mwisho

No comments: