Mwnyekiti wa taskforce Mh.Edward Haule ambaye pia diwani wa kata ya Ibumi akimpa mkono wa shukrani Askofu Simalenga
Askofu Simalenga akiwa na kamati maalumu(task force)ambayo inaandaa mchakato wa uanzishwaji wa Dayosisi mpya itakayotambulika kwa jina la Mount Living stone
KANISA
Anglikana Dayosisi ya Kusini Magharibi mwa Tanganyika jimbo la
Njombe limeanza mchakato wa kuligawa jimbo hilo na kuunda Dayosisi
mpya ya Mount Livingstone itakayokuwa na makao yake makuu wilayani
Ludewa.
Akizungumza
jana katika uzinduzi wa kamati maalum(task force) inayoratibu
kuanzishwa kwa doyasisi mpya itakayopewa jina la Mount Livingstone
Askofu mkuu wa Dayosisi ya kusini magharibi mwa Tanganyika jimbo la
Njombe John Simalenga alisema sababu ya kuligawanya jimbo ni kutokana
na ukubwa wa jimbo lililopo.
Askofu
Simalenga alisema lengo kuu la kuanzishwa kwa Dayosisi ya Mount
Livingstone itakayokuwa na makao yake makuu mjini Ludewa ni kusogeza
huduma za kimwili na kiroho karibu na watu kufuatia dayosisi ya
kusini magharibi mwa Tanganyika kuwa na eneo kubwa,jambo linaloongeza
mzigo mkubwa katika kutoa huduma.
Aidha
aliwataka washiriki katika mchakato huo kuongozwa na roho mtakatifu
kwa kujawa na hekima, uzalendo upendo na busara ili kufanikisha zoezi
hilo gumu na kulitaja eneo linalomilikiwa na Dayosisi yake kuwa ni
pamoja na eneo lote la wilaya ya Ludewa, Makete, Njombe, Mufindi
katika mkoa wa Iringa na Mlimba katika mkoa wa Morogoro.
Simalenga
alisema kutokana na mzigo ambao Dayosisi anayoisimamia kuwa mkubwa
imelazimu kuanzisha Dayosisi nyingine ili kuwasogezea waamini huduma
ya kiroho jirani kwani Dayosisi ya kusini magharibi mwa Tanganyika
imekuwa na eneo kubwa hali inayofanya usimamizi wa maeneo hayo kuwa
mgumu.
Naye
mratibu wa mchakato wa uanzishwaji wa Dayosisi ya Mount Livingstone
Kenani Andrew Hiluka alisema kimsingi vigezo vya kuanzishwa kwa
Dayosisi mpya wilayani Ludewa yamekamilika na kutaja baadhi ya
vigezo kuwa ni pamoja na uwepo wa wakristu wa kutosha, ukubwa wa eneo
linalokusudiwa kuanzishwa.
Vigezo
vingine ni kuwepo sanduku la posta/mawasiliano ya simu na miundombinu
ya barabara, kuwepo na vyombo vya usafiri, kuwepo nw uwakili
kuongezeka kwa waumini ilikukua kwa kanisa, kuwepo na wahudumu wa
kutosha, kuwepo majengo ya ofisi na nyumba ya Askofu na fedha
shilingi milioni 10 katika akaunti.
“Tuna
kila sababu ya kuanzisha Dayosisi nyingine kutokana na ukubwa wa eneo
na wingi wa waamini hivyo kwa sasa tuko katika vikao vya mwanzo ili
kukamilisha mchakato wa uanzishwaji wa dayosisi itakayotambulika kwa
jina la Mount Livingstone na makao makuu ya Dayosisi hiyo yatakuwa
Ludewa mjini”,alisema kenani Hiluka
Askofu
Simalenga aliwataka viongozi na waamini wa dhehebu la Anglikana
walioko wilaya ya Ludewa kuwa na mshikamano katika kufanikisha zoezi
hilo kwani kuna taskforce ambayo imeundwa kushughurikia mchakato huo
mpaka utakapo kamilika.
Doyasisi
mpya ya mount livingstone yenye makao makuu yake mjini Ludewa
inaundwa na mitaa/parokia 26 na kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2011
Doyasisi mpya ina jumla ya waumini 32,800.
mwisho
No comments:
Post a Comment