Mwenyekiti na muhasibu wa CWT wilaya ya Ludewa wakiwa na nyuso za furaha baada ya kushinda uchaguzi
Mhasibu mpya wa CWT wilaya ya Ludewa mwalimu Frolian Mtweve Mvanginye akiwa na furaha baada ya kushinda uchaguzi
Mwenyekiti mteule wa CWT wilaya ya Ludewa mwalimu Dominicus Mganwa baada ya kushinda uchaguzi
wajumbe wa chama cha walimu wilaya ya Ludewa wakiwa katika uchaguzi
Chama cha walimu
(CWT)wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe hatimaye kimefanikiwa
kuwapata viongozi wapya kupitia uchaguzi uliofanyika jana katika
ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo kutokana na viongozi wa awali
kustaafu na mwingine kupandishwa daraja.
Katika uchaguzi huo
wanachama mbalimbali wa chama hicho waliweza kugombea uongozi katika
ngazi ya mtunza hazina na mwenyekiti wa wilaya kwa kunadi sera zao
kwa wajumbe waliohudhuria mkutano ili waweze kuziba nafasi hizo mbili
na kupata washindi.
Akisoma matokeo ya
uchaguzi huo katibu wa CWT mkoa wa Njombe Bi.Luya Ngonyani alizitaja
sababu za kufanyika kwa uchaguzi huo ni kutokana na aliyekuwa mhasibu
wa chama hicho Ignas Mkechi kustaafu katika utumishi wa umma na
aliyekuwa mwenyekiti mwalimu Wiliam Kunyanja kuchaguliwa kuwa mjumbe
wa kamati kuu ya CWT kupitia mkoa wa Njombe.
Bi.Ngonyani alisema
kutokana na nafasi hizo kuwa wazi kwa muda mrefu na kufuatana na
katiba ya chama cha walimu Tanzania imelazimu kuchagua viongozi
wengine kupitia mkutano mkuu wa wilaya wa chama hicho ili kuziba
nafasi hizo.
“Katiba yetu inaruhusu
kufanya uchaguzi kutokana na nafasi hizi zilizoachwa wazi hivyo kila
mmoja ambaye ni mwanachama wa CWT anahaki ya kugombe na kuwa kiongozi
katika chama chake lakini kwa kuwapata viongozi hawa ninahaika
mmewachagua viongozi waadilifu na watendaji kazi wazuri na si
vinginevyo”,alisema Bi.Ngonyani.
Katika uchaguzi huo ngazi
ya uenyekiti wagombea walikuwa wane na matokeo yalikuwa kama
ifuatavyo wapiga kura walikuwa 129 kura moja ilifaribika,Nzangwa
Silingo alipata kura 3,Paulo ndimbo alipata kura 5,Ramon Lugome
alipata kura 54 na Dominicus Mganwa alipata kura 65 hivyo kumfanya
Dominicus Mganwa kuibuka kidedea na kuwa mwenyekiti wa CWT wilaya ya
Ludewa.
Kwa ngazi ya Uhasibu kura
zilizopigwa zilikua 129 ambapo Paulo ndimbo hakupata kitu,Elizabeth
Suka alipata kura 3,George Martin 3,Amina haule 6,Mathayo Tematema
kura 10,Aloysi Kapelela alipata kura 39 na Frolian Mtweve Mvanginye
alipata kura 68 kwa matokeo hayo yalimfanya mwalimu Frolian Mtweve
Mvanginye kuibuka kidedea na kupata nafasi ya Uhasibu wa CWT Ludewa.
Aidha Mhasibu mteule wa
CWT wilaya ya Ludewa mara baada ya kuchaguliwa akiwashuguru wa Jumbe
Mwalimu Frolian Mtweve Mvanginye alisema cheo hicho ni dhamana hivyo
bila ushirikiano wa wajumbe hao hakuna ufanisi wowote wa kazi utakao
undelea.
Bw.Mvanginye aliwataka
wajumbe kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kutetea maslahi
yao kwa mwajiri kwani umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu hivyo kwa
umoja wa walumu wote Tanzania hakuna kitakacho shindikana.
Nae Mwenyekiti mteule
mwalimu Dominicus Mganwa aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua na kutaka
ushirikano daima baina ya wajumbe ili kubuni miradi mbalimbali
itakyoweza kukiendesha chama hicho tofauti na michango wanayokatwa
walimu hao kila wakati.
Mwalimu Mganwa alisema
ifike wakati chama cha walimu Tanzania licha ya kupigania haki za
wanachama kwa waajiri wao lakini kila wilaya kuwe na miradi endelevu
itakayo wanufaisha wanachama katika kupata mikopo mbalimbali yenye
riba nafuu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment