SHULE msingi
nyingi wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe zinakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya
wanafunzi.
Hata hivyo
changamoto hiyo inadaiwa kusababishwa na ongezeko la idadi ya wanafunzi kwa
shule za msingi nchini,takwimu za kitaifa zinaonesha kuwepo na ongezekeko la
asilimia 40.31 la wanafunzi kwa kipindi cha mwaka 2002 hadi 2011.
Mwenyekiti
wa kamati ya shule ya msingi Madunda Bw.Chrisantus Haule alisema kuwa licha ya
shule hiyo ya zamani kumilikiwa na kanisa Katoliki lakini bado miundombinu ya
maji haina,hali inayosababisha wanafunzi kwenda kuchota maji kwenye mifereji
iliyo mbali na shule,ambayo hata hivyo si safi na salama kwa ajili ya kunywa.
Baada ya
kupata elimu kupitia mradi wa maji,Afya na usafi wa mazingira unaoendeshwa na
shirika la Daraja,uongozi wa shule kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji
wamelipa kipaumbele suala hilo kwa kuanza na mkakati wakuchemsha maji na
kuyahifadhi katika majaba kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi ili kuwanusuru na
maambukizi ya homa za matumbo na kuhara.
Ofisa elimu
vielelezo wilaya ya Ludewa Bi.Helena Halifa aliwasisitiza walimu,wazazi na
wanafunzi kuthamini utamaduni wa kuchemsha maji ya kunywa majumbani na ,shuleni
ili kuwaepusha watoto na magonjwa yatokanayo na kunywa maji machafu,pamoja na
kuzingatia usafi wa kunawa mikono kila wanapotoka choooni,hatua ambayo alisema
itasaidia kupunguza gharama za matibabu.
“Jamani hili
suala halihitaji gharama na ni kwaajili ya watoto wenu wenyewe,sasa usipolea mtoto
wako unadhani nani atakulelea?Tupunguze matumizi yasiyo ya lazima tuweke hili
suala mbele”,alisema Bi.Halifa.
Pamoja na
kuwa maji huwa ya msimu katika eneo hilo,wazazi pamoja na walimu wameamua
kutafuta maji kwa gharama yoyote pasipo kuwahusisha watoto wao ambao wanatakiwa
kuwa darasani saa zote za masomo.
“Sisi
tutapangiana zamu kulingana na vitongoji vyetu na tutajua jinsi gani tutachota
maji na kuyaleta shuleni,wakati tukisuburi mkakati wa muda mrefu wa kuyafikisha
maji shuleni”,alisema Bw.Joseph Kayombo,mmoja wa wazazi katika eneo hilo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment