Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

June 28, 2013

DIWANI AZUIA TANKI LA MAJI HUKU WANANCHI WAKIHANGAIKA NA MAJI.



.Mbunge aingilia kati na kuwapelekea wananchi

DIWANI wa Kata ya Masasi wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe Laurance Mahundi amelalamikiwa na wananchi wake kwa kuzuia tanki la maji walilopewa na mbunge wao na kisha kulitelekeza katika yadi ya ujenzi tangu mwezi februari mwaka huu huku akishinda kucheza bao mjini wakati wananchi wakiteseka na maji.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili wananchi wa kata ya Masasi walisema Julai 18 mwaka 2011 mbunge wao Deo Filikunjombe alifika katika kata yao kwania ya kuwashukuru na ndipo wakamweleza shida wanazokabiliana nazo ikiwemo uhaba wa maji unaosababishwa na ukosefu Tanki la kutunzia maji.

””” sisi wananchi wa kata ya masasi tunatumia maji yaliyopo katika mtandao wa maji ya mchuchuma manda na mabomba yakitoboka na maji kuanza kupotea huwa tunapata shida sana lakini kama tungekuwa na Tanki la kuhifadhia maji tusingekuwa na shida ya maji. Alisema kiongozi wa ngazi ya kata ambaye hakupenda jina lake liandikwe 

Stanley Gowele ni katibu wa mbunge wa Ludewa kwa upande wake alikiri kuwa wananchi wa masasi walimwomba mbunge awasaidie tanki la maji kwa ajili ya kuhifadhi maji kutokana na mabomba kutoboka kila wakati huku wao wakikumbwa na adha ya maji na kulazimika kunywa maji yasiyosalama.

Gowele akaongeza kuwa disemba 2012 mbunge alipata Tanki Dar es salaam na kulituma hadi Njombe na februari mwaka huu alikodi gari kwa ajili ya kulipeleka tanki hilo hadi kata ya masasi lakini diwani akataka lishushwe mjini Ludewa atalipeleka yeye.

,,,, Februari mwaka huu mimi nilikodi gari kwa ajili ya kulisafirisha tanki la maji kutoka njombe hadi kata ya masasi lakini nilipompigia simu diwani alipokee akajibu kuwa yeye yuko safari na kuagiza lisipelekwe bila yeye hivyo lishushwe atalipeleka kwa gari la halmashauri ndiyo lipo mpaka sasa.’’’’ Akasikitika sana Gowele

Alipoulizwa kwanini alizuia tanki hilo lisipekwe na kwa nini hajapeleka hadi sasa diwani Mahundi alijibu kwa kebehi kuwa siyo kazi ya mbunge kupeleka tanki katika kata yake na kwamba atalipeleka muda ukifika bila kutaja na muda gani aliopanga kupeleka tanki kwa wananchi walioliomba.

Naye kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Gladness Mwano alisema kuwa hana taarifa kuhusu kucheleweshwa kwa tanki hilo lakini akaahidi kufuatilia taarifa hizo kwa mhandisi wa maji wilaya ili kujua kwanini tanki limeendelea kuwepo badala ya kuwapelekea wananchi mali yao

Masasi ni kata inayokabiliwa na uhaba wa maji kutokana na kuwa na miundombinu isiyo ya uhakika. Hata hivyo katibu wa mbunge wa Ludewa Stanley Gowele aliahidi kulipeleka tanki la maji haraka ili kuwanusuru wananchi hao.

             mwisho

No comments: